Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe Leo January 20, 2023 amesema Wilaya anayoiongoza ilipokea kiasi cha fedha za Kitanzania Billion 5/= kutoka Serikali Kuu kwa Mwaka 2022 kwa lengo la Ujenzi wa miundombinu ya shule
Ameyasema hayo katika kikao cha tathimini ya utekelezaji wa shughuli za uboreshaji na usimamizi wa elimu Mkoa wa Kigoma kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Adengenye
Katika kikao hicho amesema Wilaya ya Kigoma imetelekeza Ujenzi wa Shule Mpya za Sekodari tatu (03) kwa Kata ambazo awali hazikuwa na Shule za Sekondari kwa gharama ya fedha za Kitanzania Million 470/= kwa kila Shule kutokana na mradi wa Sequip na ujenzi wa vyumba vya madarasa mia mbili na tatu (203)
Kwa Mwaka wa fedha 2022/2023 Manispaa ya Kigoma/Ujiji ilipokea kiasi cha fedha za Kitanzania Million 470/= kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa Sequip kwa lengo la ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Businde ambapo tayari imeanza kutumika
Aidha fedha zingine zilizopokelewa ni kiasi cha fedha za Kitanzania Billion moja na milion mia moja arobaini na Sita (Tsh 1, 146, 000, 000/=) kutoka Serikali Kuu kwa lengo la ujenzi wa vyumba vya Madarasa 57 kwa maandalizi na mapokezi ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa Mwaka 2023
Manispaa hiyo iliendelea kupokea fedha zilizotokana na makato ya miamala ya simu( Tozo) kiasi cha Tsh 37, 500, 000/= na kiasi cha fedha Tsh 100, 000, 000/= zilizotumika katika ukamilishaji Maabara, Ukamilishaji wa maboma ya madarasa Tsh 200, 000, 000/= kwa Shule za Msingi na Sekondari
Wilaya ya Kigoma inaundwa na Halmashauri mbili, Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa