Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma Leo Februari 28, 2025 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Ziara hiyo imefanyika ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Kigoma Ndugu. Jamal Tamim kwa lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama.
Mwenyekiti kwa niaba ya kamati ya Siasa amepongeza ubora wa miradi ya maendeleo na usimamizi unaofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi inayojengwa kwa fedha za Kitanzania Million 180/=, Ujenzi wa vyumba vinne (04) vya Madarasa na matundu sita (06) ya Vyoo Shule ya Msingi Buronge kwa gharama ya fedha za Kitanzania Million 117.2/=, na Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Kata ya Kipampa kwa gharama ya Tsh Million 603/=.
Aidha miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na Ukarabati wa MV Liemba, Chanzo cha Maji kilichopo Kibirizi, na Ujenzi wa barabara ya Shani kwa kiwango cha Lami iliyopo Kata ya Buzebazeba
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa