Na Mwandishi Wetu
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigoma Jana Desemba 20, 2022 walifanya ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa 57 unaoendelea Manispaa ya Kigoma/Ujiji ikiwa ni ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya chama hicho
Katika ziara hiyo Viongozi na Wajumbe wa Kamati hiyo waliridhishwa na ujenzi huku wakipongeza usimamizi wa Wataalamu chini ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo
Manispaa hiyo ilipokea kiasi cha fedha za Kitanzania Billion moja na milion mia moja arobaini na Sita (Tsh 1, 146, 000, 000/=) kutoka Serikali Kuu kwa lengo la ujenzi wa vyumba hivyo vya Madarasa ikiwa ni maandalizi na mapokezi ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa Mwaka 2023
Akizungumza Katika ziara hiyo Katibu wa itikadi uenezi wa CCM Wilaya ya Kigoma Ndugu. Haruna Kambiro aliwapongeza Wataalamu wa Manispaa hiyo kwa Usimamizi wa ujenzi wa Madarasa kwa Shule kumi na sita (16) huku akiwataka kuendelea kukamilisha ili kuwanufaisha wanafunzi pindi Shule zitakapofunguliwa
Mjumbe wa Kamati hiyo na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Mhe. Kilumbe Shabani Ng'enda alisema ujenzi wa miundombinu hiyo unaendelea kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya Madarasa katika Manispaa hiyo na kufanya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya upili kuanza kwa wakati mmoja
Mjumbe wa Kamati hiyo na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe aliwataka Wananchi kuitunza Miundombinu hiyo kwa kutoruhusu uhalibifu wowote huku akiwataka Wazazi kuhakikisha kila Mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na masomo ya upili anaripoti kwa wakati
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athumani Msabila alisema ujenzi wa vyumba vya Madarasa unaendelea kukamilishwa katika hatua za mwisho ili kuanza kutumika mapema mwezi Januari 2023
Alihitimisha kwa kusema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali na inatarajia kuleta fedha zingine za Maendeleo katika Ujenzi wa Miundombinu ya vyumba vya Madarasa kwa Shule za Msingi kupitia mradi wa Boost
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa