Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi mkuu wa manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu.Kisena Mabuba amewataka Viongozi wa elimu kuongeza ufaulu wa Wanafunzi katika Mitihani ya ndani na ya Kitaifa.
Ameyasema hayo Leo Januari 09, 2026 alipokuwa akiongea na Maafisa elimu Kata, Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari, na Walimu wa TEHAMA katika mafunzo ya mfumo wa kidigitali wa taarifa za Shule (BEMIS SIS) yanayoendelea Shule ya Sekondari Kigoma.
Amewataka Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule kusimamia suala la ufundishaji na kukuza ufaulu kwa kila shule usiopungua asilimia tisini na tatu (93%) katika mitihani ya Kitaifa na kudhibiti utoro wa Walimu na Wanafunzi.
Aidha ameahidi kutoa motisha kwa kila mwalimu na Shule zitakazokuwa zikiongeza ufaulu katika Mitihani ya Kitaifa.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa