Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Kigoma Jana April 03, 2023 ilitembelea miradi iliyotekelezwa na inayotekelezwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa mwaka wa fedha 2022/2023
Ziara hiyo ilifanyika ikiongoza na Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Kigoma Mhe. Ahmed Mwilima kwa kutembelea na kukagua miradi tisa (09) katika Kata mbalimbali za Manispaa hiyo
Kamati hiyo ilitembelea ujenzi wa Hospitali ya Manispaa inayoendelea kujengwa Kata ya Kagera ambapo tayari Serikali imeleta fedha za awali kiasi cha Tsh 500, 000, 000/=, Ujenzi wa Zahanati tatu (03) za Kata ya Machinjioni, Kibirizi na Kamala, na kutembelea Ujenzi ambao umeshakamilika katika Shule ya Sekondari Rubuga
Aidha miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Kipampa unaoendelea ambapo Serikali inatarajia kuendelea kujenga Majengo mapya kupitia mradi wa Sequip kwa gharama ya Tsh 573,000, 000/=, Ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Buhanda unaendelea kujengwa kupitia mapato ya ndani, na kutembelea miradi ambayo imekamilika Shule ya Sekondari Businde, Kituo cha afya cha Gungu, na Ujenzi wa shedi soko la Kamala-Bangwe
Mwenyekiti huyo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigoma aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo imeendelea kutoa fedha za miradi ya maendeleo na kuupongeza uongozi wa Manispaa kwa namna wanavyotekeleza miradi kupitia mapato ya ndani
Alipongeza Wataalamu kwa namna wanavyosimamia utekelezaji wa miradi kwa kusogeza huduma za kijamii karibu na Wananchi katika sekta ya afya, elimu, na kukuza uchumi wa Wananchi kwa kutoa ajira kipindi cha utekelezaji wa miradi hiyo
Zaidi endelea kutembelea Tovuti www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa