Na Mwandishi Wetu
Waratibu elimu Kata, Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari, na Walimu wa TEHAMA Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo Januari 07, 2026 wameanza mafunzo ya siku (04) ya mfumo wa kidigitali wa taarifa za Shule (BEMIS SIS).
Akifungua mafunzo hayo Afisa elimu Takwimu Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Felix Kitanga amewataka Washiriki kuzingatia mafunzo yatakayosaidia kuanza kutumia Mfumo wa Basic Education Management Information System Students Information System (BEMIS SIS) kutumia na kuwasilisha taarifa za Shule katika Mamlaka mbalimbali.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Bakari Abdi amesema Mfumo huo wa kielekroniki utakuwa chachu ya maendeleo katika sekta ya elimu.
Amesema mfumo huo unasaidia upatikanaji wa taarifa za Shule kwa wakati ikiwemo taarifa ya miundombinu ya Shule, maazimio na maandalio ya Walimu, Mahudhurio ya walimu na Wanafunzi, kupunguza kazi za makaratasi na kuongeza uwazi na uwajibikaji.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa