Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amewataka Watumishi wa Manispaa hiyo kuongeza juhudi na Ufanisi katika kutoa huduma kwa Wananchi.
Ameyasema hayo Leo Januari 09, 2026 katika kikao chake alichokifanya na Watumishi kikihusisha Wakuu wa Idara na Vitengo, Watumishi wa Makao makuu na Watendaji wa Kata za Manispaa hiyo.
Amewataka kusimamia na kutekeleza malengo ya kila idara na taasisi huku akitangaza kila Mwezi kuanza kupatikana mfanyakazi bora na kupata motisha ya zawadi na fedha kutokana na namna alivyotoa huduma katika utumishi wake.
Amewataka Watumishi hao kuendelea kutekeleza Mfumo wa kieletroniki wa Upimaji utendaji kazi (PERPEMIS) kwa kujaza Shughuli zinazotekelezwa na kufanya tathimini kwa Watumishi waliochini yao.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa