Na Mwandishi Wetu
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) ameagiza Viongozi wa Serikali na Kisiasa zao la Michikichi kuwa agenda yao ya Kudumu katika vikao, Mikutano na katika kuwahamasisha Wananchi
Ameyasema Leo February 26, 2023 katika kikao cha Wadau wa zao la Michikichi kilichofanyika Ukumbi Wa NNSF uliopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji kikihusisha Viongozi wa Serikali, Wanasiasa , taasisi, wazalishaji wa mbegu za michichikichi, wamiliki wa viwanda vidogo vya kuchakata mazao na bidhaa za michikichi pamoja na wakulima wakubwa na wadogo wa zao hilo
Katika kikao hicho Waziri Mkuu amesema zao la Michikichi ni fursa kwa Wakulima na Wananchi waliopo Mkoani Kigoma kutokana na Serikali kuweka zao hilo kuwa miongozi mwa mazao ya Kimkakati Nchini
Kiongozi huyo amesema Mkoa wa Kigoma unazalisha 80% ya Michikichi inayolimwa Nchini na Kusema Serikali itaendelea kuwekeza katika kuinua zao hilo kwa lengo la kuinua maisha ya Wakulima, Wasindikizaji, Wafanyabiashara na Wamiliki wa Viwanda
Kiongozi huyo amewataka Wakulima kulima zao hilo kwa kupanda mbengu za Kisasa ambazo Miaka miwili tangu kupandwa huanda kuzaa matunda
Amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo kusimamia Maafisa kilimo waliopo kupangiwa maeneo ya Kata na vijijini kwa lengo la kukaa karibu na Wakulima ili kuendelea kutoa elimu na kukagua mashamba ya wakulima
Aidha ameagiza Halmashauri kushirikiana na taasisi zingine zinazozalisha miche kwa kuzipatia fedha kwa lengo la kuzalisha na kugawiwa kwa Wakulima wa Halmashauri Husika bure
Amehitimisha kwa kumtaka Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya kufuatilia kwa karibu Miche ya michikichi wanayogawiwa Wakulima na kuweka mipango ya elimu na kufanya vikao vya mara kwa mara ya tathimini ya zao hilo
Naibu Waziri Wa Kilimo Mhe. Antony Mavunde amesema katika kuinua zao la Michikichi Mkoani Kigoma tayari Serikali imetenga fedha za kwa ajili ya Ujenzi wa maabara ya Utafiti, Ofisi na nyumba za Watumishi katika kituo cha Utafiti wa zao la Michikichi Kihinga
Amesema katika kukuza zao la Michikichi Serikali inatarajia kuweka ruzuku ili kurahisisha upatikanaji wa miche ya kisasa kirahisi na kwa wakati ili kuokoa kiasi cha fedha kinachotumika kuagiza mafuta ya kula Nje ya Nchi huku akiwashauri wakulima Kujikita katika mashamba Makubwa na ya pamoja
Nchini Tanzania kwa sasa Mahitaji ya Mafuta ya Kula ni zaidi ya Tani 650, 000 huku uzalishaji unakakadiriwa kuwa tani 290, 000 na kiasi cha tani 360, 000 sawa na 55% huagizwa kutoka Nje ya Nchi na kugharimu Serikali kiasi cha fedha za Kitanzania Billion 470 kila Mwaka
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa