Na Mwandishi Wetu
Menejimenti ya Wakuu wa Idara na Vitengo (CMT) Manispaa ya Kigoma/Ujiji wamefanya ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na inayotarajia kutekelezwa katika Manispaa hiyo.
Ziara hiyo imefanyika Leo Februari 25, 2025 ikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa Ndugu. Kisena Mabuba huku akiitaka Menejimenti kusimamia miradi kikamilifu.
Viongozi hao wamefanya ziara katika eneo ambalo jengo la Utawala linatarajia kujengwa kwa Tsh billion 3/= hadi kukamilika ambapo hadi sasa Halmashauri imeshapokea kiasi cha fedha za Kitanzania Billion 1/= kutoka Serikali Kuu.
Viongozi hao watembelea ujenzi wa Shule ya Sekondari Mpya inayoendelea kujengwa eneo la Burega Kata ya Buzebazeba kwa gharama ya zaidi ya Million mia sita (Tsh 603, 890, 663.00/=) kwa kujenga miundombinu ya vyumba vya madarasa, Jengo la Utawala, Matundu ya vyoo, maabara 03 za Sayansi, Maktaba, Chumba cha TEHAMA, pamoja na tenki la Maji.
Miradi mingine iliyotembelewa ni ujenzi wa nyumba ya Walimu ya Shule ya Sekondari Mjimwema kwa gharama ya Tsh 110, 000, 000/= ikiwa imefikia hatua ya upauaji, Ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi kwa gharama ya Tsh 180,000,000/= ikiwa hatua ya umaliziaji na kutembelea eneo linalotarajiwa kujengwa ukumbi wa kisasa kwa gharama ya fedha za Kitanzania Billion Tatu (Tsh 3,000, 0000, 000/=) hadi kukamilika.
Zaidi bofya www.kigomaujiji.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa