Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamis Kali Leo June 22, 2023 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu kwa shule za msingi kupitia mradi wa BOOST wenye thamani ya fedha zaidi ya billion moja (Tsh 1, 467, 200,000/=) inayotekelezwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Kiongozi huyo amefanya ziara hiyo akiambatana na Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya huku wakiridhishwa na kupongeza namna ujenzi wa miundombinu ya madarasa inavyotekelezwa
Mkuu wa Wilaya ameitaka ofisi ya Mkurugenzi kuhakikisha wanasimamia thamani ya mradi na kukamilisha kwa wakati
Ujenzi huu unahusisha ujenzi wa Shule tatu (03) mpya unaoendelea kujengwa kwa gharama ya Tsh 922,600,000/=, Ujenzi wa Madarasa kumi na sita (16) kwa gharama ya Tsh 416,000,000/=, Ujenzi wa madarasa 2 ya elimu ya awali ya mfano kwa gharama ya Tsh 71,800,000/=, Ujenzi wa darasa 1 la elimu maalumu Tsh 26,000,000/=, na Ujenzi wa matundu kumi na nne (14) ya vyoo kwa gharama ya Tsh 30,800,00/=
Shule zinazotekeleza mradi huu ni pamoja na Ujenzi wa Shule mpya Kiheba iliyopo Kibirizi kwa gharama ya Tsh 561,100,000/= na Ujenzi wa Shule mpya ya Kibirizi kwa gharama ya Tsh 361,500,000/=
Ujenzi wa madarasa manne (04) Shule ya Msingi Katubuka kwa gharama ya Tsh 104,000,000/=, Ujenzi wa darasa moja (01) la Wanafunzi wenye Mahitaji maalumu kwa gharama ya Tsh 26,000,000/= na ujenzi wa Matundu matatu (03) ya vyoo kwa gharama ya Tsh 6,600,000/=
Shule ya Msingi Kabingo inatekeleza ujenzi wa madarasa manne (04) kwa gharama ya Tsh 104,000,000/=, na Ujenzi wa matundu manne (04) ya vyoo kwa gharama ya Tsh 8,800,000/=,
Aidha Shule ya Msingi Kipampa inaendelea na ujenzi wa madarasa manne (04) kwa gharama ya Tsh 104,000,000/=, na Ujenzi wa matundu matatu (03) ya Vyoo kwa gharama ya Tsh 6,600,000/=
Pia, Shule ya Msingi Butunga inatekeleza ujenzi wa madarasa manne (04) kwa gharama ya Tsh 104,000,000/=, Ujenzi wa madarasa mawili (02) ya awali ya Mfano kwa gharama ya Tsh 71,800,000/=, na Ujenzi wa matundu manne (04) ya vyoo kwa gharama ya Tsh 8,800,000/=
Endelea kutufuatilia kupitia mitandao yetu ya kijamii na tovuti kwa kubofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa