Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamis Kalli Leo Novemba 30, 2023 amefungua mafunzo ya Siku tano(05) kwa Wasaidizi wa Watoto Mahakamani yanayofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Katika Ufunguzi huo Mkuu huyo wa Wilaya amewataka Wataalamu wanaohusika na uendeshaji wa kesi za Ukatili kwa Watoto kuzifanyia uamuzi kwa wakati mara pindi ushahidi unapokamilika.
Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Wasaidizi wa Watoto Mahakamani katika kufuatilia mashauri, Upatikanaji wa haki za Msingi kwa Wakati, mashauri kufanyika mda wowote hata kama kuna changamoto kwa wazazi au Walezi, Kuandaa Mtoto wakati wa kesi, kuhakikisha sauti ya Mtoto inasikika wakati wa mashauri ( kujieleza kwa jambo lolote kwa kujiamini) , na kueleza kwa niaba ya Mtoto.
Katika ufunguzi huo mafunzo hayo yamehudhuriwa na Katibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa idara na Vitengo, Mahakimu, na Waendesha Mashtaka /Mawakili.
Sheria ya Mtoto kufungu cha 94. Ni jukumu la Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha haki na ustawi wa Mtoto zinapatikana, kulindwa pamoja na kuendelezwa.
Zaidi www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa