Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua amepokea Vifaa vya maabara za Sayansi kutoka Shirika la Watoto Duniani (UNICEF) na baadae kukabidhi kwa Wakuu wa Shule za Sekondari Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Kiongozi huyo amepokea Vifaa hivyo vya Shule 95 za Mkoa wa Kigoma kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa vikigharimu kiasi cha fedha zaidi ya Billion moja na million Mia mbili.
Mara baada ya kupokea vifaa hivyo, Kiongozi huyo amekabidhi kwa Wakuu wa Shule za Sekondari 11 za Manispaa ya Kigoma/Ujiji ambazo ni Shule ya Sekondari Kigoma, Businde, Masanga, Buronge, Kitwe, Buteko, Katubuka, Mwananchi, Kichangachui, Kasimbu na Buzebazeba.
Vifaa hivyo vitasaidia kurahisisha ujifunzaji na ufundishaji kwa masomo ya Sayansi na kukuza viwango vya ufaulu katika masomo ya Fizikia,Kemia , Biologia na Hisabati.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa