Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamis Kali Jana Septemba 04, 2023 aliongoza Mkutano wa Wadau wa mradi wa uboreshaji Usalama wa milki za ardhi Unaotekelezwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Mkutano huo ulifanyikia katika Ukumbi wa Redcross ukishirikisha Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa idara na Vitengo, Viongozi wa dini, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Waandishi wa habari, Wakuu wa Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali kwa lengo la kujadili na kutoa maoni ya utekelezaji wa mradi huo
Àwali Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Evans Mdee akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo alisema hadi Sasa Katika Kata ya Kibirizi jumla ya Makazi 4000 yametambuliwa huku michoro na ramani ya viwanja 1500 ikiwa imeandaliwa kwa Wananachi wa Mtaa wa Kibirizi,
Aliwataka Wajumbe wa Mkutano huo kuendelea kutoa maoni ya utekelezaji wa mradi huo utakaotatua kero na migogoro ya umiliki wa ardhi, mipaka na matumizi ya ardhi
Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji katika Kata za Kibirizi, kasingirima, Kagera, Gungu, Businde, Rubuga, Majengo, Kitongoni na Kasimbu wanatarajia kunufaika na kupanga, kupima, kusajiri upataji wa hati miliki za ardhi zaidi ya elfu kumi (10,000) bure katika Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki Ardhi na kusimika mfumo wa kielektroniki wa kuhifadhi kumbukumbu za ardhi
zaidi endelea kufuatilia kupitia tovuti ya www.kigomaujijimc.go.tz na katika Mitandao ya kijamii ya Facebook na Instgram kwa jina la #kigomaujijimc
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa