Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma/Ujiji Dr. Rashid Chuachua ameongoza Wananchi na Wafanyabishara katika Soko la Nazareth Manispaa ya Kigoma/Ujiji kufanya usafi kuelekea siku ya Mazingira Duniani.
Mkuu wa Wilaya amewataka Wananchi kuzingatia suala la Usafi ili kuboresha afya zao na kuepukana na matumizi ya mifuko ya Plastiki inayoleta athari hasi kwa Mazingira.
Maadhimisho ya kilele cha siku ya Mazingira Duniani hufanyika kila mwaka June 05, na Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni "Mazingira yetu na Tanzania ijayo tuwajibike sasa, Dhibiti matumizi ya plastiki".
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa