Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Kali Leo May 30, 2023 amewataka Viongozi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kutopokea misaada yenye masharti ya kupotosha maadili ya Kitanzania ili kutekeleza Majukumu yao
Ameyasema hayo katika kikao cha Mwaka cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Majukumu yake Manispaa ya Kigoma/Ujiji kilichofanyikia Ukumbi wa Joy in the Harvest
Ameyataka Mashirika kutoa elimu ya malezi yaliyosahihi kwa jamii ili kuwa na watu wenye maadili ya Kitanzania
Aidha ameyataka Mashirika kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Shughuli zao kila robo ofisi kwa lengo la kufuatilia shughuli zinazotekelezwa na vyanzo vya mapato
Awali Mratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Austina Hwago Akisoma taarifa Amesema Manispaa ya Kigoma/Ujiji ina jumla ya Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali hamsini na nne (54) ambapo kwa Mwaka 2022/2023 yametumia kiasi cha Tsh 462, 700, 750/= huku zaidi ya Wakazi 12, 958 wakinufaika na miradi mbalimbali
Katika kikao hicho Viongozi hao wamepatiwa mafunzo ya elimu ya ulipaji kodi na misamaha kwenye taasisi za kiraia pamoja huku baadhi ya Mashirika yakipokea vyeti vya pongezi kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa