Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamisi Kali amewataka Wenyeviti wa Serikali Za Mitaa kusimamia usalama katika maeneo yao ya utawala kwa kushirikiana na kamati za usalama Kata na Wilaya
Ameyasema hayo Leo February 16, 2023 alipokutana na Wenyeviti hao ikiwa ni Mara ya Kwanza Mara baada ya kuanza kazi katika Wilaya hiyo
Kiongozi huyo amesema suala la Usalama wa mitaa inapaswa kuwa agenda ya kudumu katika vikao vyao na katika mikutano ya Wananchi
Amewataka viongozi hao kwa kushirikiana na Wananchi kubaini wanaofanya vitendo vya uharifu katika maeneo yao na wahamiaji haramu na kutoa taarifa katika vyombo vya usalama
Aidha amewataka viongozi hao kusimamia na kuhamasisha Wananchi kushiriki usafi wa mji katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kusimamia na ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ya Utawala
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Kasulu uliopo Kata ya Kasingirima Ndugu. Mlekwa Mfaume amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kufanya kikao na Wenyeviti hao wa Serikali za Mitaa huku akisema wataendelea kushirikiana na Serikali katika kusimamia miradi ya maendeleo, usalama wa Wananchi na kuhamasisha usafi wa mji
Manispaa ya Kigoma/Ujiji ina jumla ya Kata kumi na tisa (19) na jumla ya Mitaa sitini na nane(68)
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa