Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe. Salum Hamis Kali amewataka Madiwani wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kuendelea kuielimisha jamii kwa kushirikiana na Wataalamu ili kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji
Ameyasema hayo Leo April 13, 2023 wakati akihutubia Mkutano wa Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo ambapo pia ameshauri Baraza hilo kutunga sheria ndogo zitakazosaidia kupambana na vitendo vya ukatili na kuwa na jamii inayozingatia maadili na utamaduni wa Kitanzania
Amewataka Waheshimiwa Madiwani kwa kushirikiana na Wananchi kupinga viashiria na vitendo vya ukatili kwa kutoa taarifa kwa wakati katika mamlaka zinazohusika na hatua za kisheria kuchukuliwa
Aidha amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kufuatilia Vituo vya malezi, Taasisi, na Mashirika yasiyo ya Serikali yaliyosajiriwa katika Halmashauri hiyo ili kujiridhisha na shughuli zinazotekelezwa
Aidha amewataka Madiwani hao kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata mbalimbali za Manispaa hiyo kwa lengo la kuwanufaisha Wananchi
Amehitimisha kwa kuwataka kuendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa Wananchi kujikita katika kulima zao la Kimkakati Michikichi ya kisasa ili kukuza uchumi wa jamii na mtu moja moja
Zaidi www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa