Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salumu Kali, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo February 28, 2023 wametembelea familia za Kata ya Kagera kwa kutoa pole kutokana na kufiwa kwa Watoto waliozama katika mto Luiche kutokana na Mtumbwi kuzama
Viongozi hao wamefika katika Kata hiyo Mapema Asubuhi wakiambatana na Kamati ya Ulinzi na Upsalama Wilaya ya Kigoma, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Viongozi wa dini walioongoza Sara ya faraja kwa wafiwa
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salumu Kali amewapongeza Wavushaji wa Mto Ruiche, na Wanachi kwa ushirikiano ambao wameendelea kufanya tangu siku ya kwanza katika jitihada za kuokoa watoto waliozama kwa kushirikiana na Jeshi la zimamoto na ukoaji
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa maboya kumi (10) yatakayokuwa yakitumika katika kivuko hicho kuwavusha wanafunzi wa ishirini na Moja (21) ambao bado wanasoma Shule ya Msingi Kagera huku akiwataka wazazi kuwaruhusu watoto wao kuhudhuria masomo
Amelitaka Jeshi la Zimamoto na Ukoaji kuendelea na Jitihada za kusaka mwili ambao bado haujapatikana
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Mhe. Kilumbe Ng'enda Shabani ameitaka Serikali kuharakisha Ujenzi wa barabara ya Wafipa-Kagera itakayojumuisha ujenzi wa daraja la mto Ruiche ili kuondokana na Changamoto za ajari pamoja na changamoto za usafirishaji mazao
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athumani Msabila amesema Serikali inatekeleza Ujenzi wa barabara ya Wafipa-Kagera ya km 2 itakayojumuisha ujenzi wa daraja la Mto Ruiche kupitia Mradi wa TACTICS unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB)
Siku ya Ijumaa February 24, Mwaka huu Mtubwi uliokuwa umebaba Wanafunzi sita (06) ulizama katika Mto Ruiche ambapo wawili waliokolewa wakiwa hai, Siku ya Jumamosi miili miwili ya Wanafunzi waliofatiki ilipatikana na Mwili Mmoja umepatikana leo February 28, 2023 na kufanya miili ya Watoto watatu (03) kupatikana na kikiso cha zimamoto na ukoaji kinaendelea na jitihada za kuutafuta mwili wa mtoto mmoja ambao haujapatikana mpaka sasa.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa