Msanii wa Bongo fleva Nasibu Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platinum leo desemba 30, ameahidi kutoa meza mia moja (100) kwa wafanyabiashara wa soko la Kigoma night market kutokana na wafanyabiashara hao bidhaa zao kuzitandaza chini pindi wanapokuwa katika soko hilo
Msanii huyo ameyasema hayo alipokutana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo ikiongozwa na katibu tawala wa mkoa huyo Ndugu. Rashidi Mchata kwa niaba ya Mkuu wa mkoa, uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji na wasanii alioambatana nao msanii huyo Diamond
Akiongea katika kikao hicho msanii huyo amesema amekuja kusheherekea miaka 10 ya Mafanikio katika mziki anaoufanya na hadi sasa jamii imeupokea vizuri kutokana na vijana kujingizia kipato binafsi, kuendesha familia na kulipa kodi mbalimbali za serikali kutokana na sanaa hiyo
Ameendelea kusema kwa sasa kuna mambo ambayo tayari ameyafanya katika mkoa wa Kigoma kama mwanzo tu kutokana awali kutokuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na uongozi wa serikali, na kusema tayari amejenga visima vinne (4) vya maji safi, ujenzi wa msikiti wa Azizi na madrasa na kusema ataendelea kuisaidia jamii katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na kukuza vipaji vya sanaa kutoka kwa vijana wa mkoa huo
Msanii huyo ameipongeza Shirika la Reli Tanzania(TRC) kwa ushirikiano waliopewa katika safari waliyoianza kutoka Mkoa wa Dar es salaam hadi kufika Kigoma na kusema ni maendeleo makubwa sana na uwekezaji unaofanyika katika shirika hilo kwa kiwango cha standard garge na kuahidi atarudi kwa treni hiyo msanii huyo akiwa na timu yake yote
Amehitimisha kwa kuwashukuru wakazi wa mkoa wa Kigoma kwa kujitokeza kwa wingi katika mapokezi aliyoyapata jana desemba 29 alipofika na kuvishukuru vyombo vya usalama kwa ulinzi ambao wameupata na ambao wanaendelea kuwataka huku akiwataka kushirikana hadi watakapokuwa wakiondoka kurejea jijini Dar es salaam
Naye katibu Tawala wa Mkoa huo Ndugu. Rashidi Mchata awali akimkaribisha katika mkoa huo amempongeza kwa kuja kusheherekea miaka kumi nyumbani akiwa katika sanaa ya mziki huo na kusema wako tayari kumpa ushirikiano katika maeneo atakayopita na matamasha atakayoyafanya katika suala la ulinzi na usalama
Akiendelea kutoa taarifa za maendeleo ya mkoa huo amesema mkoa wa Kigoma umeendelea kuimarika katika miundondombinu ya barabara kama vile barabara zilizozengwa manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa ufadhili wa Benki ya Dunia, kuongezeka kwa hali ya ufaulu na uandikishaji kwa wanafunzi ambapo amesema kwa mwaka 2018 uandikishaji ulipanda kwa 83% na ufaulu kwa mtihani wa kidato cha nne 2015-2019 umepanda kutoka 71% hadi 83% na ufaulu wa kidato cha sita kutoka 89% hadi 99.25%
Pia amamtaka msanii huyo kuendelea kuutangaza mkoa wa Kigoma kwa kuwakaribisha wageni kuja kuweza katika mkoa huo lakini pai kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo kwa kutumia kampuni ya Wasafi yenye vyombo vya habari radio na televisheni kama vile hifadhi ya Gombe na Mahare, meli ya Liemba, majumba ya makumbusho na uhifadhi wa ziwa Tanganyika
Amehitimisha kwa kumtaka msanii huyo kuwa balozi wa Tanganyika Bussnes Summit , ambalo ni kongamano la kibaiashara linalohusisha mikoa jirani ya mkoa wa Kigoma na nchi jirani ikiwemo Burundi, Rwanda, Zambia na Congo katika kujadili namna ya ukusaji biashara na uwekezaji katika mkoa wa Kigoma.
Aidha Mbunge wa viti maalumu anayewakilisha Vijana Bungeni Mhe. Zainabu Katimba amempongeza msanii huyo kwa mafanikio aliyonayo tangu aanze sanaa ya mziki na kusema ni chachu kubwa kwa vijana wengine kujifunza kutoka kwa msanii huyo katika Nyanja za maisha mbalimbali
Ameendelea kuwataka wasanii wote na viongozi mbalimbali kuendelea kuunga mkono serikali ya awamu ya Tano kwa jitihada zinazozifanya katika kuboresha mazingira ya vijana na Watanzania wote serikali inafikia malengo yake iliyoyakusudia ili kuboresha maisha ya wananchi wote
Msanii huyo anatarajia kufanya tamasha katika uwanja wa Lake Tanganyika Usiku wa Desemba 31, ikiwa kiingilio ni Bure kwa kuwashukuru wakazi wa mkoa huo kwa kumshika mkono ndani ya miaka kumi hadi mafanikio aliyonayo na tamasha hilo linatarajiwa kuhudhuliwa na watu mbalimbali wa mkoa huo wakiwemo wageni kutoka nchi jirani Burundi, Congo na Rwanda
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa