Na Mwandishi Wetu
Diwani wa kata ya Kigoma Mhe. Baraka Lupoli leo Desemba 9, amechaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji katika kura zilizopigwa na waheshimiwa Madiwani wa Manispaa hiyo mara baada ya kula kiapo cha kutumikia nafasi hizo katika ukumbi wa NSSF Kigoma
Uchaguzi huo umefanyika sambamba na kumchagua Naibu Meya ambapo Diwani wa Kata ya Kipamba Mhe. Bi Mgeni Omary Kakolwa ameibuka mshindi katika nafasi hiyo huku kamati za kudumu za Madiwani zikiundwa ili kuanza kufanya kazi
Kabla ya Uchaguzi huo Madiwani hao waliapishwa na Kamishiana wa Viapo na baadae kutoa Tamko la ahadi ya Uadilifu kwa viongozi wa Umma kwa mjibu wa sheria kutoka kwa viongozi wa Tume ya Maadili
Akihutubia Mstahiki Meya mara tu baada ya kuapishwa amewataka Madiwani kuvunja makundi ya kisiasa kutokana na uchaguzi huo kuisha na kuanza kuwa watumishi wa Wananchi kwa kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika kata kumi na tisa za Manispaa huku wataalamu Kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo wakitoa ushirikiano katika kutatua kero na changamoto za Wananchi
Mstahiki Meya huyo ameahidi kufanya ziara za kushitukiza mara kwa mara katika Kata na Mitaa ya Manispaa hiyo kwa kukagua utekelezaji wa Ilani ya Awamu ya Tano na kuhakikisha watendaji wanakuwepo mda wote katika maeneo ya kazi na kushughulikia maendeleo ya wananchi
Jumla ya Madiwani waliokula kiapo ni Ishirini na Tano (25), kumi na tisa (19) waliochaguliwa na wananchi kutoka katika Kata za Manispaa na Madiwani sita (06) wakiwa ni Madiwani Miti Maalumu na Sherehe hizo za Uapishwaji wa madiwani zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kisiasa, Serikali na dini akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma , Mbuge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mameya Wastaafu, viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wawakilishi kutoka katika Mabenki, Wananchi na Waandishi wa Habari
Video na picha ya tukio hili tembelea Maktaba ya picha katika tovuti yetu www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa