Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chua chua Leo Oktoba 04, 2024 ameiongoza kamati ya ulinzi na usalama kufanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji iliyopo Kata ya Kagera.
Mkuu wa Wilaya hiyo akiwa katika ukaguzi huo amewataka Wataalamu kuendelea kutumia mfumo wa kielekroniki wa manunuzi katika kupata Wazabuni katika Shughuli za Ujenzi.
Amesema Kamati ya Ulinzi na usalama inaendelea kutembelea miradi mbalimbali katika Manispaa hiyo kwa lengo la kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali zinawanufaisha Wananchi kwa kujenga na kutoa huduma katika viwango bora.
Akiwa katika ziara hiyo ameongea na Wagonjwa wa nje waliokofika kupata huduma za Matibabu huku akiipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa namna ambavyo imeendelea kuboresha huduma za afya.
Manispaa ya Kigoma/Ujiji ilipokea Kiasi cha fedha za Kitanzania Billion Moja na Million Mia tatu (Tsh 1, 300, 000, 000/=) kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje ambalo limekamilika na linatumika, Jengo la Maabara, Jengo la Wazazi (Maternity Complex), Jengo la mionzi, na Stoo ya dawa ambapo Ujenzi bado haujakamilika.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa