Na Mwandishi wetu
Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji imendelea kutoa elimu ya kujikinga na Ugonjwa wa Corona katika taasisi za dini huku waumini wakishukuru juu ya elimu hiyo waliyoipata
Elimu hiyo imetolewa leo March 21 katika kanisa la Waadventista wasabato Mwasenga ambapo jumla ya Waumini wakubwa sabini na sita(76) na watoto sabini na saba (77), huķu kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKT) Mlole watoto wadogo 180 wakipata elimu hiyo
Mganga na Mratibu wa Ukimwi katika Manispaa hiyo Dr.Shabaan Magorwa amewataka waumini hao kuzingatia kanuni za kujiepusha na Ugonjwa wa Corona kwa kuepuka na kuachana na utamaduni wa kusalimiana kwa mikono, kuachana na tabia ya kukumbatiana na kubusiana kwa kipindi hiki cha ugonjwa huu
Katika semina hiyo waliyoipata wamekumbushwa kuhakikisha suala la usafi linazingatiwa, huku wakiaswa kunawa mara kwa mara kwa maji yanayotiririka na sabuni ili kuweza kupambana na virusi vya corona
Aidha mganga huyo ameendelea kusema ugonjwa wa corona ni hatari kwa afya na kuzorotesha uchumi kutokana na namna mgonjwa aliyepata ugonjwa anavyohudumiwa "kwa kweli ugonjwa huu unadhorotesha uchumi kutokana na gharama ya vifaa tiba, idadi ya madaktari wanaomuhudumia mgonjwa mmoja ni gharama kubwa jambo ambalo linaweza kuathiri uchumi wetu, hivyo tufate kanuni ili tuweze kuepukana na ugonjwa wa corona " Amesema Daktari huyo
Ameendelea kuwataka jamii kutoa taarifa sahihi katika mamlaka zinazohusika na kuitaka jamii kuachana na tabia za wale wanaodanganya kuwa na ugonjwa huo na kuzua taharuki kwa wengine huku akisema anayesadikika kuwa na ugonjwa huo lazima awe na historia ya kusafiri kutoka nje ya nchi au amekutana na wageni
Ameendelea kuwataka viongozi wa Makanisa hayo kutojenga dhana potofu juu ya Ugonjwa huo ukilinganisha na wachungaji wanaoleta taharuki kwa waumini wao na kuwanywesha baadhi ya madawa ambayo sio maalumu kwa kunywa na kuhatarisha afya zao na kuwataka watumie mda wao kuliombea taifa kuhusu Ugonjwa huo
Naye Mzee wa Kanisa wa Kanisa la Waadventista wasabato Mwasenga Ndugu. Sauli Malekela ameshukuru kwa elimu hiyo iliyotolewa huku akisema wao kama viongozi wa kanisa hilo hawataleta taharuki kwa waumini wao bali kuendelea kutoa elimu kwa mjibu wa Wizara ya Afya na kusema wao kama kanisa wameweka utaratibu wa kuweza kuombea Taifa kuepukana na athari zinazoweza kutokana ugonjwa huo na kuwaombea Watanzania sita (6) ambao tayari wamegundulika kuwa na ugonjwa huo
Nao baadhi ya waumini wa kanisa la Waadventista wasabato akiwemo Ndugu. Batholomeo Bizoba amesema elimu waliyoipata ni mhimu sana na wataifanyia kazi kwa kuzingatia kanuni za afya na wao kutoa elimu hiyo kwa watu wengine huku wakoshukuru Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kwa kuwapelekea elimu hadi Makanisani
Zaidi ya wagonjwa 11,000 yatari wamekwishafariki duniani kutokana na Ugonjwa wa Corona na wagonjwa 250,000 wamepatikana na virusi vya Ugonjwa huo ambao ni ugonjwa unaoshambulia mfumo wa kupumua huku Tanzania wagonjwa 6 wamethibitishwa kuwa na ugonjwa huo pasipo kuwa na vifo
Picha zaidi ingia katika maktaba ya picha
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa