Na Mwandishi Wetu
Wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo March 27, 2024 wametoa elimu ya upumzishwaji shughuli za Uvuvi Ziwa Tanganyika na ufugaji wa Samaki kwa njia ya Vizimba.
Elimu hiyo imetolewa Katika Ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ikihusisha Mkuu wa Wilaya, Mbunge, Mkurugenzi, Madiwani , Wataalamu wa Uvuvi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi, Watendaji kata na Mitaa wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Akizungumza katika Kikao hicho Mtaalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi Ndugu. Ndasisye amesema upumzishwaji wa Shuguhuli za Uvuvi ziwa Tanganyika unatarajia kufanyika kwa kupindi cha miezi mitatu kuanza May 15, hadi Agosti 15, 2024 kutokana na Azimio la Nchi za Congo, Zambia, Burundi na Tanzania ili kuleta tija ya ongezeko la Samaki na Dagaa.
Amesema kwa sasa elimu inaendelea kutolewa kwa Wadau mbalimbali ikiwemo Wananchi na Wavuvi kwa kufanya vikao katika mialo kwa kuhamasishaji wa ufugaji kwa njia ya vizimba vinavyotarajia kutolewa na Wizara hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Kali amewataka Wadau wa Uvuvi na Wananchi kuwa Wavumilivu katika kipindi cha miezi mitatu ili kuwa na tija katika mazao ya Uvuvi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja ameitaka Wizara ya mifugo na Uvuvi kuendelea kutoa elimu na upatikanaji wa haraka wa Vizimba ili ufugaji uanze mara moja kwa Wavuvi na Wananchi wa Manispaa hiyo.
Mkoani Kigoma pekee, Uvunaji wa Samaki umepungua kutoka Tani 26, 568. 59 zenye thamani ya Shilingi bilion 132.84 Mwaka 2020 hadi kufikia Tani 15, 531. 82 zenye thamani ya Shilingi bilioni 108. 72 Mwaka 2023 Sawa na upungufu wa Asilimia 42, upungufu umechangiwa na Sababu mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa nguvu ya Uvuvi, matumizi ya zana haramu za uvuvi na mabadiliko ya tabia ya Nchi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa