Na Mwandishi Wetu
Shirika la Enabel limetambulisha mradi wa Wezesha binti kwa Wakazi na Wananchi wa Kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Zoezi la utambulishaji mradi limefanyika Leo Desemba 12, 2024 katika eneo la Soko la Kagera kwa kufanya mkutano na Wananchi.
Akiwasilisha Mada katika Mkutano huo Mratibu wa Mradi wa Wezesha binti Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Neema Bugemwe amesema Mradi wa Wezesha binti katika Kata ya Kagera unatarajia kutekeleza Ujenzi wa Bweni la Wasichana na Vyoo vya kisasa katika Shule ya Sekondari Wakulima.
Amesema mradi unalenga kuwawezesha Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu wenye umri wa Miaka 14-29 kupata elimu ya upili katika hali ya usalama.
Mradi wa Wezesha Binti unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (Enabel) ambapo pia mradi utawaimarisha Wavulana na Wasichana katika utunzaji wa mazingira, kujifunza Ujasiriamali na upatikanaji wa ajira.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa