Na Mwandishi Wetu
Shirika la Enabel limetoa Vipeperushi vya Utoaji elimu ya kupinga ukatili ikiwa ni katika maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia.
Vipeperushi hivyo vilikabidhiwa Jana Septemba 02, 2024 vikipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Ndugu. Richard Mtauka ambapo alilishukuru Shirika hilo huku akisema vifaa hivyo vitatumika katika muendelezo wa kampeni ya kupinga ukatili katika jamii na taasisi.
Akikabidhi vifaa hivyo Mtaalamu wa Jinsia na Ushirikishwaji wa Jamii kutoka Shirika la Enabel Bi. Jovita Mlay alisema vifaa hivyo vimegharimu kiasi cha fedha za Kitanzania Million Tatu(Tsh 3,000,000/=) vikitoa ujumbe wa kuhamasisha Jamii kushiriki kupinga na kutokomeza vitendo vya ukatili.
Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia hufanyika Kila Mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa