Na Mwandishi wetu
Wakuu wa Idara na Vitengo Manispaa ya Kigoma/Ujiji wametakiwa kuwawezesha kuwainua wananchi kiuchumi kwa kuwapatia elimu ya uchakataji wa taka zinazozalishwa katika Manispaa hiyo
Ushauri huo umetolewa na Mtaalamu wa Mazingira na uchakataji taka Ndugu. Patrick Matandala kutoka kampuni ya Belgium Development Agency wakati akitoa Mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika kuanzia March 29-30,2021 katika Ukumbi wa Hoteli ya Greenview namna ya udhibiti na upunguzaji wa taka mjini
Mtaalamu huyo amesema zipo fursa mbalimbali ambazo wananchi wanapaswa kuzifanya kutokana na taka zinazalishwa, kusanywa na kupelekwa dampo la kisasa la Msimba ambapo kwa sasa fursa kubwa ni pamoja na utengenezaji wa mbolea ya Mboji na mbolea za viwandani kwa ajili ya wakulima wa ndani na nje ya mji huo
Ameendelea kusema fursa zingine ni pamoja na kubadili matumizi (Recycling) na kutumika tena (Re-use) kwa vitu kama vile plastiki na chuma ili kuhakikisha gharama za usafirishaji wa taka unapungua na mji unakuwa safi kutokana na taka hizo kutumika kwa namna nyingine bora
Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya kigoma/Ujiji na Mkuu wa idara ya Mipango miji na Ardhi Ndugu. Brown Nziku amewaomba wawekezaji kuja kuwekeza katika Manispaa hiyo na kuchangamkia fursa za ugeuzaji taka kuwa malighafi zingine zinazoweza kutumika kwa matumizi mengine ya binadamu kutokana na uzalishaji wa taka kuwa mkubwa
Kaimu Mkurugenzi huyo amewataka wananchi kuunda vikundi vya wajasiriamali na kuvisajili ili viweze kuwezeshwa kupata mikopo isiyokuwa na riba na kuhakikisha wananchi kupitia vikundi hivyo wanachangamkia fursa hizo ikiwa ni pamoja na uzoaji taka katika mitaa na makazi ya watu ili kuhakikisha mji unakuwa safi na watu kujiajiri na kuzalisha ajira ya kazi hiyo
Wataalamu hao wamehitimisha mafunzo hayo kwa kufanya ziara katika vizimba vya ukusanyaji taka na kutembelea kikundi cha Umoja kinachopatikana kata ya Gungu eneo la veta wanaojishughulisha na uchakataji wa taka za plastiki kwa kuzisaga na kusafirisha bidhaa hiyo kwa ajili ya Masoko katika Jiji la Dar es salaam
Inakadiriwa kuwa kwa kila mkazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji anazalisha kilogram 0.5 kwa siku na Kwa sasa Manispaa ya Kigoma/Ujiji inazalisha tani mia moja na arobaini (140) za taka kwa siku na uzalishaji huo umekuwa ukikua kutokana na hali ya ukuaji wa mji kwa ongezeko la idadi ya watu
Picha na video zaidi bofya http://www.kigomaujijimc.go.tz/sinlge-gallery/vifaa-na-mafunzo-ya-usafi-na-mazingira-kutoka-kwa-kampuni-ya-lawatama
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa