Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mwailwa Pangani leo January 2, 2019 amemtaka mhariri mkuu wa gazeti la Mwananchi kumuomba msamaha kutokana na kuchapisha habari ya uongo .
Ameyasema leo ofsini kwake alipokuwa na mkutano wa waandishi wa habari kutokana na habari ya desemba 31,2018 katika gazeti la mwananchi iliyomhusisha mkurugenzi huyo kwa kumtuhumu katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Humpley Polepole kusababisha kushusha mapato ya halmashauri hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari ofsini kwake Mkurugenzi huyo amesema alishitushwa na habari hiyo iliyo nukuu maneno yake na kumtaja kwa jina wakati hajawahi kufanya mahojiano na mwandishi wa habari hiyo.
Ameendelea kusema chanzo cha habari hiyo ni mgogoro wa wafanya biashara baina yao na halmashauri juu ya utoaji wa ushuru wa pango kwa wafanyabishara kushindwa kulipia pango kwa Tsh. 50,000/= na katibu wa uenezi kutoa ushauri kwa manispaa ya Kigoma Ujiji kuhusiana na pango hilo kuwa chini ya kiwango hicho jambo kwa kubadilisha sheria ndogo za utoaji ushuru huo.
Ameendelea kusema serikali ilimaliza mgogoro huo kupitia TAMISEMI kwa kutoa Mwongozo wa namna wafanyabiashara wa masokoni watakavyokuwa wakilipa ushuru wa pango ambapo iliamuliwa kwa masoko madogo kulipia Tsh 15000/= kwa kila duka kwa mwezi, na kwa masoko makubwa kulipia ushuru wa pango Tsh 25000/= kwa kila duka kwa mwezi.
Ameendelea kusema mgogoro huo haukushusha mapato bali uliongeza wigo kwa watendaji kuibua vyanzo vipya vya mapato na kufanya mapato kuongezeka zaidi kwa kipindi hiki ukilinganisha na kipindi cha mgogoro huo.
“huduma za wananchi zimeboreshwa stendi kuu ya mabasi taa zinawaka usiku na mpango ulikuwa taa za barabara ya kutoka mjini kwenda ujiji ziwake changamoto imekuwa wizi uliotokea kwa nyaya za barabarani lakini kwa sasa hali iko vizuri na tumeibua vyanzo vingine vya mapato vilivyokuwa vinapotea kama sabuni zinazotengezwa Kigoma, chanzo cha mawese na ushuru wa madini kama vile mawe na kokoto” ameyasema Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi huyo ameendelea kueleza namna halmashauri ilivyoweka mazingira mazuri wa wafanyabiashara wa mashuka kwa kuwaonesha eneo la soko la Ujiji kufanyia biahara hiyo kwa lengo la usalama kwa wafanyabiashara hao tofauti na awali kufanya biashara kando ya barabara za lami jambo ambalo linahatarisha usalama wa maisha yao.
Amemaliza kwa kusema mpango wa watendaji ni kuendelea kukusanya na kukuza zaidi mapato ya halmashauri hiyo na kufikia lengo la kukusanya million 200.8 kwa mwezi kutokana na malengo na mikakati iliyowekwa kwa mjibu wa bajeti .
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa