Na Mwandishi Wetu
Wajumbe wa Kamati ya Kupambana na kudhibiti UKIMWI Halmashauri ya Mji wa Kibaha ya Mkoani Pwani Wamepatiwa mafunzo namna ya Kupambana na kuzuia maambukizi ya UKIMWI kutoka kwa Wajumbe wa Kamati hiyo Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Mafunzo hayo yametolewa Leo Septemba 01, 2023 katika Ukumbi wa Kigoma Social Hall mara baada ya Kufika kufanya ziara ya Kujifunza namna Manispaa ya Kigoma/Ujiji ilivyofanikiwa kudhibiti Maambukizi ya UKIMWI kutoka 2.9% hadi kufikia 2.6%
Awali Akiwasilisha taarifa Mratibu wa Udhibiti wa UKIMWI Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Raban Gwaguzo amesema jumla ya Watu wanaoishi na VVU katika Manispaa hiyo ni Watu 5,257 wanaume wakiwa 1,662 na Wanawake 3,595 kati ya Wakazi 322,524 kwa mjibu wa Sensa ya Watu na Makazi 2023 na hali ya Maambukizi yakiwa ni kwa 2.6%
Amesema mikakati ya Kupunguza Maambukizi kwa Manispaa hiyo ni pamoja na kuendelea kutoa huduma za Upimaji wa VVU , kutoa tiba na mafunzo kwa Watu wanaoishi na VVU katika vituo vya kutolea huduma za afya
Ameendelea kusisitiza mikakati mingine ikiwa ni pamoja na kuendelea kugawa kondomu katika Maeneo ya Nyumba za kulala Wageni, kutoa elimu kwa makundi yaliyohatarini, kudhibiti maambukizi ya Mama kwenda kwa mtoto na kutoa huduma ya tohara kwa Wanaume katika vituo vya afya
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Dr. Peter Nsanya amesema Halmashauri hiyo inaendelea na mapambano ya kudhibiti UKIMWI ambapo kwa sasa hali ya Maambukizi ni 3.2% na Mkoa wa Pwani kwa ujumla hali ya maambukizi yakiwa kwa 5%
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa