Halmashauri ya manispaa ya kigoma ujiji leo july 26, imepongezwa kwa kuongeza mapato ya ndani kwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Pongezi hizo zimetolewa na wageni kutoka Benki kuu na Ofisi ya Rais-TAMISEMI walipokutana na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri na wakuu wa idara baada ya ziara yao ya siku nne ya kufatilia utendaji kazi na ukaguzi wa mahesabu katika miradi ya Uendelezaji miji na Majiji kimkakati Tanzania ( TSCP) unaofadhililiwa na benki ya dunia (WB).
Akiiongea katika kikao hicho Ndugu. Evans Mgeusa mhasibu wa mradi wa Uendelezaji wa Miji na Maji Kimkakati Tanzania(TSCP) kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI amewapongeza wataalamu wa halmashauri hiyo kwa kuibadilisha halamshauri hiyo kimaendeleo katika usimamizi wa miundombinu mbalimbali.
Ameendelea kusema kadri ujenzi wa miundombinu ya barabara na masoko unavyoendelea kukua usababishe kuboreka kwa maisha ya wakazi wa manispaa hiyo jambo litakaloleta matokeo makubwa katika ongezeko la kipato cha halmashauri nakuweza kujiendesha bila shida ya aina yeyote.
Ameendelea kusema halmashauri ina wajibu wa kusimamia vyanzo vya mapato vilivyopo na kuendelea kuibua vyanzo vipya vya mapato katika kuhakikisha halmashauri inajiendesha bila kuwa na vikwazo vya kifedha na kuweza kuboresha huduma za wananchi kama vile afya, elimu na uchumi.
Naye mtaalamu wa maswala ya fedha kutoka Benki kuu Ndugu. Nkundwe Mwakiluma katika kikao hicho ameipongeza halmashauri hiyo kwa kuongeza kipato kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kwa 36% kutoka katika mapato halisi ya billion moja na themanini na nane elfu laki mbili sitini na saba (Tsh 1,088,267,000/=) ukilinganisha kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo mapato halisi yalikuwa bilioni moja na sabini na nne elfu laki tano sabini na mbili mia nane sabini na nne (Tsh 1,074,572,874/=).
Ameendelea kusema katika ukaguzi uliofanyika wa usimamizi wa masuala ya fedha katika halmshauri hiyo wamegundua mfumo wa mapato na mfumo wa epicor uko vizuri katika uendeshaji na kuwa na viwango vinavyofanana licha ya tofauti ndogo katika mambo ya kifedha suala ambalo lilikuwa na tofauti na awali.
Ameendelea kusema kwa jitihada zinazoonekana sasa halmashauri ina juhudi thabiti za kuhakikisha hati chafu inaondoka kutokana na kupatikana kwa hati chafu hiyo kwa miaka mitatu mfulululizo “ nimeona jitihada kubwailiyofanya na Mkurugenzi wa halmashauri hii kupitia ofisi ya Mweka hazina kutaka kuondoa hati chafu iliyopo kwa vitabu ambavyo tayari vimeshafungwa na kupungua kwa hoja za ukaguzi”
Ameendelea kuwataka wataalamu kuendelea kushughulikia hoja za ukaguzi za mkaguzi wa ndani kabla ya Mkaguzi wa nje hajazifanyia kazi na kusababisha kwenda ofisi ya CAG zikiwa tayari zimejibiwa jambo litakaloiletea halmashauri hati iliyosafi.
Ameendelea kuitaka halmashauri kuboresha utendaji kazi wa ofisi ya Mkaguzi wa ndani kwa kuongeza watumishi katika ofisi hiyo ambapo ameipongeza pia GIZ kwa vifaa walivyovitoa katika ofisi hiyo kwa kutoa komputa nne laptop na printa moja katika kuleta ufanisi wa kazi.
Ameendelea kuipongeza ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa kuwa na kitengo kinachoratibu malalamiko ya miradi ya TSCP na malalamiko ya wananchi hali inayosababisha kuondoa migongana baina ya ofisi ya Mkurugenzi na wananchi wanao pitiwa na miradi katika makazi yao.
Naye kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ndugu. Emmanuel Katemi amewashukuru wageni hao kwa ukaguzi walioufanya na kuahidi kuwa halmashauri itaendelea kuboresha na kuibua vyanzo vipya huku jitihada za kuondoa hati chafu zikiendelea kufanyika.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa