Halmashauri ya Manispaa ya manispaa ya Kigoma/Ujiji jana Octoba 3, imetoa mikopo ya shilingi million mia moja na sabini(170,000,000/=) kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya serikali ya awamu ya tano.
Mikopo hiyo iliyotolewa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga kwa vikundi 46 ikiwa ni kwa mashariti nafuu ambapo watarejesha pasipo kuwa na riba yeyote.
Akitoa taarifa kaimu mkuu wa idara ya Maendeleo ya jamii wa manispaa hiyo Ndugu. Jabiri Majid alisema halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji imekuwa na utamaduni wa kuhamasisha vikundi vya wajasili amali wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuunda vikundi vya ujasiliamali kwa lengo la kuinua uchumi wa makundi hayo na kuweza kujipatia mikopo itakayokuza miradi yao.
Aliendelea kusema kwa sasa halmashauri imepiga hatua kubwa katika mapato ya ndani kutokana na mwaka jana kutoa mikopo kwa makundi hayo shilingi million ishirini tu (20,000,000/=) licha ya mikopo hiyo kuleta matokeo makubwa ya vipato kwa akina mama wanaofuma mashuka na kuuza dagaa, walemavu wanaouza vyakula na vijana wanaofanya biashara ya usafirishaji (bajaji na bodaboda).
Ameendelea kusema changamoto wanayokutana nayo ni baadhi ya vikundi vya wajasiliamali hao kutorudisha fedha hizo kwa wakati, vikundi vinavyoundwa na vijana kutaka mafanikio ya haraka na vikundi vingine kuvunjika kabla ya kurejesha na kusema kwa kipindi cha mwaka 2012 hadi 2019 milioni thelethini na tisa (39,000,000/=) hazijarejeshwa ikiwa ni wadaiwa sugu na tayari hatua ya ufatiliaji na wengine kupelekwa mahakamani imeshaanza.
Naye mjasiliamali na mwenyekiti wa dawati la uwezeshaji kwa wanawake kiuchumi Bi. Maria Kandoga akitoa salamu kwa niaba ya vikundi vingine alisema halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji imekuwa msaada mkubwa katika kuinua uchumi wa vikundi vya wajasiliamali kupitia wataalamu wake ambapo amesema watalaamu wamekuwa wakiwatembelea na kufatilia miradi wamayoifanya huku wakiwasaidia kuhusu sula la masoko.
Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Kigoma Yassin Mtalikwa aliwataka wajasiliamali hao wa vikundi fedha wanazozipata wazitumie kwa usahihi katika shughuli za kiuchumi na kuzirejesha kwa wakati huku akisisitiza serikali ya awamu ya tano kupitia chama cha mapinduzi (CCM) imejipambanua katika kuhakikisha inawasaidia makundi hayo kupitia halmashauri zote nchini.
Naye meya wa manispaa hiyo Ndugu. Hussein Ruhava akimkaribisha mgeni rasmi aliwataka wale wanaopokea mikopo hiyo wahakikishe mikopo hiyo inaleta mabadiliko katika shughuli zao za kiuchumi na kufanya uchumi unakua na kusema halmashauri itaendelea kutoa mikopo kutokana na mapato ya ndani lakini pia baraza la madiwani litasimamia mikopo hiyo inatolewa na kurejeshwa pasipo mgogoro ya aina yeyote
Naye mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga akihutubia aliipongeza halmashauri kwa utoaji wa mikopo kwa wajasiliamali hao huku akiwataka akina mama kuitumia mikopo hiyo kwa shughuli iliyokusudiwa ya ukuzaji uchumi wa familia, halmashauri na Taifa kwa ujumla
“ili kuleta tija katika kuwanufaisha wajasiliamali mikopo hiyo ambayo inatolewa na halmashauri kupitia mapato yake ya ndani ni heri kuwapatia makundi machache ya wajasiliamali fedha kubwa na kuleta matokeo makubwa kuliko kupatia makundi mengi ya wajasiliamali na fedha kidogo” alisema mgeni rasmi huyo
Aliendelea kusema katika mkoa wa Kigoma omba omba wameongezeka kwa kiasi kikubwa jambo ambalo amelipiga marufuku na kumuagiza mkuu wa wilaya hiyo ya Kigoma ombaomba atakayeonekana achukuliwe hatua na wale wanaotoa misaada wahakikishe misaada yao wanaipeleka katika vituo vya kulea watu wenye mahitaji maalumu
Alizitaka mamlaka zinazotoa vibali vya kufanya biashara nchi jirani zihakikishe zinatoa vibali haraka ili wajasiliamali wa sabuni, vitenge na mashuka waweze kupeleka nchi za Burundi, Kongo na Rwanda kwa lengo la kupanua wigo wa masoko ya vikundi hivyo vya wajasiliamali.
Akihitimisha hotoba yake aliwataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika zoezi zima la uandikishaji linaloendelea katika mkoa huo na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuchagua viongozi waliosahihi na watakaowasaidia katika kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa