Halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji jana july 4, imesainisha mikataba ya ajira kwa watoza ushuru na wafanya usafi kwa watu zaidi ya themanini katika ukumbi wa halmashauri hiyo.
Akiwahutubia waajiriwa hao Kaimu wa idara ya Utumishi Ndugu Iddy Kalingoji aliwataka katika utumishi wao watakaoufanya baada ya kujaza mikataba kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kufikia malengo yaliyokusudiwa katika halmashauri hiyo katika ukusanyaji mapato na kuhakikisha mji unakuwa safi kwa wale wafanya usafi.
Aliendelea kusema mkataba utakaokuwa unajazwa ni wa mwaka mmoja mmoja na kutokufikia malengo kwa ajira uliyopewa ndicho kipimo cha kujua utendaji kazi wako hali itakayofanya kutoendelea katika ajira hiyo kwa kipindi kingine.
Aliendelea kuwataka kuwa na maadili katika utendaji kazi katika utumishi katika matumizi ya lugha katika utendaji kazi na mwonekano wao katika mavazi yanayofaa ili kuweza kuleta ufanisi katika kazi hizo.
Naye Mwekahazina wa halmashauri hiyo akiwahutubia waajiriwa hao wa Ukusanyaji mapato aliendelea kuwasisitiza kuwa waaminifu kutokana na masuala ya ukusanyaji wa fedha baadhi ya watu kushindwa kuwa waamifu.
Aliendelea kusema watasambazwa katika vyanzo mbalimbali vya mapato vilivyopo ikiwa ni pamoja na stendi na masoko yaliyopo ndani ya halmashauri hiyo na vyanzo hivyo tayari vimefanyiwa utafiti wa viwango vyake vya fedha kwa kutumia mawakala na watendaji wa halmashauri hali itakayofanya mkusanyaji kutodanganya katika shughuli hiyo.
Aliendelea kusema ajira hizo walizopata watoza ushuru lengo ni kuleta mapinduzi ya ukusanyaji mapato makubwa ukilinganisha na kipindi cha awali walipokuwa wakitumia watendaji na mawakala katika ukusanyaji huo.
Naye kaimu wa kitengo cha Tehama Yona Kisusi akizungumza katika ukumbi huo na wakusanya mapato alisema wakusanya mapato hao watapewa mashine za ukusanyaji mapato(POS) ambazo ndizo zitakazotumika kuwapa risti wateja watakao kuwa wanalipa ushuru na tozo zingine.
Aliendelea kusema katika matumizi ya mashine hizo za ukusanyaji mapato (POS) wamekuwepo watu ambao sio waaminifu kwa kujaribu kuibia mapato halmashauri kupitia mashine hizo jambo ambalo ni hatari zaidi na atakayefanya hivo atachukuliwa hatua.
Aliendelea kusema “tayari mbinu zinazotumika katika kuiba mapato ya halmashauri kupitia mashine za kukusanyia mapato tumeshazijua ikiwa na baadhi kutoa ripoti badala ya risti halali, na wengine kuzima data pindi wanapokuwa katika ukusanyaji mapato hakikisha usifanye hivo na uhakikishe unakuwa makini kwa kutumia mashine kwa usahihi maana kama ukienda kinyume tutakubaini na kukuchukulia hatua”.
Naye afisa afya wa manispaa Ndugu. Chobaliko akizungumza na wafanya usafi aliwataka kuhakikisha mji unakuwa msafi na unakuwa katika hali ya ushindani na miji mingine huku akiahidi kutoa vifaa vya usafi na kuwasambaza katika maeneo mbalimbali ya usafi katika manispaa hiyo ikiwa ni pamoja na masoko, stendi za halmashauri .
Nao baadhi ya waajiriwa wakizungumza katika ukumbi huo Ndugu. Bundala Joseph mtoza ushuru na zubeda Richard mfanya usafi waliishukuru halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kutoa fursa za ajira hali itakayopunguza vijana wengi kujiingiza katika makundi yasiyofaa kutokana na ukosefu wa ajira.
Picha zaidi ingia www.kigomaujijimc.go.tz katika maktaba ya picha.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa