Na Mwandishi Wetu
Hospitali ya Manispaa ya kigoma/Ujiji imewekewa jiwe la Msingi huku zoezi la uzinduzi wa utoaji wa huduma kwa Wagonjwa wa Nje ukifanyika Leo February 19, 2024.
Zoezi hilo la Uwekezaji wa jiwe la Msingi na uzinduzi wa kuanza kwa huduma limefanyika na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Thobias Adengenye huku likihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Vyama vya Siasa, Serikali na Wananchi.
Katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo imeendelea kuleta fedha za Mìradi ya Maendeleo zaidi ya Billion kumi na Moja (Tsh Billion 11. 450/=).
Mkuu huyo wa Mkoa amewataka Wananchi kutunza miundombinu iliyopo huku akisema Serikali imeleta fedha za Ujenzi wa Chuo Kikuu kishiriki Tawi la Mhimbili na kinatarajiwa kujengwa eneo hilo la Kagera.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja amesema kwa kipindi cha Awamu ya Sita Serikali tayari imeleta Kiasi cha Billion tatu na million Mia tatu (Tsh Billion 3.4/=) katika Ujenzi wa Miundombinu katika Sekta ya Afya.
Amesema kuanza kwa huduma katika Hospitali hiyo kwa Wagonjwa wa Nje Watumishi kumi (10) Watakuwa wakitoa huduma ya Matibabu huku akiahidi kuendelea kusimamia nidhamu ya Watumishi katika Hospitali hiyo.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa