Na Mwandishi Wetu
Kituo cha afya cha Buhanda kilichopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji kimeanza kutoa huduma ya upasuaji kwa Wajawazito wanaopata uchungu pingazi.
Huduma hiyo imeanza kutolewa Leo Februari 14, 2024 mara baada ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kuwezesha vifaa tiba vya zaidi ya fedha za Kitanzania Million mia tatu (Tsh Million 300/=) katika kituo hicho cha afya.
Huduma hiyo ya upasuaji ya kwanza imesimamiwa na Mganga Mkuu wa Manispaa Dr. Hashim Mvogogo chini ya Dr. Festus Bavuma, Dr Ally Said Abdallah, na Mtaalamu wa dawa za usingizi Pastory Simon huku mtoto wa kiume akizaliwa.
zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa