Na Mwandishi Wetu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philip Mpango amefanya uzinduzi wa jina la barabara ya Dr. Jane Goodal ikiwa ni kuenzi mchango wake wa kulinda na kuhifadhi Mazingira Mkoani Kigoma.
Akizindua jina la barabara Kiongozi huyo amesema Dr. Jane Goodal ana mchango mkubwa katika kuendeleza Viumbe hai na kuitangaza hifadhi ya Taifa ya Gombe ambayo imekuwa kivutio cha Watalii wengi Mkoani Kigoma.
Aidha Amewataka Watanzania na Wananchi wa Manispaa ya KigomaUjiji kuendelea kutunza na kuhifadhi Mazingira kwa upandaji miti.
Akizungumza katika uzinduzi huo Meya wa Manispaa ya Kigoma/ Ujiji Mhe. Baraka Naibuha Lupoli amesema barabara hiyo awali ilikujulikana kwa jina la Barabara ya Kibirizi.
Zaidi www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa