Katibu mkuu utumishi na maadili ofsi ya Rais Rocky Robert Setembo jana june 18 ametoa mwaliko kwa Afisa malalamiko manispaa ya Kigoma Ujiji kuhudhulia mkutano wa wadau wa public sector system strengthing(ps3) utakaofanyika Morogoro june 25, na 26.
Alitoa mwaliko huo katika kikao kilichomhusisha Dr. Peter M. Kilima kutoka ps3 Dar es salaam, Moses Musolezi katibu tawala msaidizi mkoa wa Kigoma, mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma ujiji, afisa utumishi, afisa wa mipango miji, ardhi na maliasili, afisa Tehama,afisa wa mipango na uchumi pamoja na afisa malalamiko.
mwaliko huo aliutoa baada ya kukagua na kulidhika na kazi nzuri inayofanywa na Afisa malalamiko wa manispaa hiyo ndugu Mellagi S. Mollel kutokana na mpangilio alioufanya wa rejesta ya kushugulikia malalamiko, na kumtaka afisa malalamiko huyo kujiandaa kutoa mada na namna ya kushugulikia malalamiko na mpangilio wa nyaraka za kushugulikia malalamiko .
naye Dr. Peter M.Kilima alisema ofsi ya public sector system strengthing(ps3) wameandaa miongozo ya kushugulikia malalamiko na maadili ya watumishi wa umma, na kuendelea kusema ofsi ya malalamiko lazima ifanye kazi kwa ufanisi na kushugulikia malalamiko ambapo alisema “kama mtu au kiongozi yeyote halalamikiwi hawezi jua kama anakosea”.
Ameendele kusema lazma wananchi na watu wengine wenye malalamiko kupewa elimu ili kujua hatua za kupitia katika kushugulikia malalamiko, licha ya wengine kutohitaji kufuata hatua hizo na amesema “hata kama kuna malalamiko yamefika ngazi za juu aidha kwa mkurugenzi ni mhimu yarudishwe kwa afisa malalamiko kwa lengo la kufuata hatua.
Katibu mkuu huyo kutoka ofsi ya utumishi na maadili ofsi ya Rais ndugu Rocky Robert Setembo licha ya kushugulikia na kitengo cha malalamiko alifuatilia kitengo cha habari kupitia tovuti ambapo alisifia kazi inayofanywa na Afisa habari na kumtaka kufanya kazi na idara zote na kumtaka mkurugenzi wa manispaa Dr. John Shauri Tlatlaa kuzitaka idara kumpa ushirikiano afisa habari huyo
Katika kukagua utendaji kazi wa tovuti katibu mkuu wa utumishi na maadili ofsi ya Rais akishirikiana na Dr.Peter M. Kilima waliweza kusifia mwonekano wa tovuti hiyo, kusifia habari zilizopo kuwa ni za wakati ukilinganisha na baadhi ya tovuti za halmashauri nchini.
Naye afisa habari wa manispaa hiyo ndugu Fred E. Bilintyo aliweza kuelezea baadhi ya changamoto zinazoikabili katika uendeshaji wa tovuti ikiwa ni pamoja na habari kushindikana pandishwa kwa wakati kutokana na mpangilio wa tovuti ulivyo(backend), baadhi ya wakuu wa idara kutompatia ushirikiano wa kutosha katika utendaji kazi ambapo amesema ni tatizo lililokuwa likiikabili manispaa kwa mda kwa sababu awali hapakuwepo afisa habari , lakini wanaendelea kutoa elimu kupitia ofsi ya mkurugenzi.
Lakini pia wametaka wakuu wa idara , kutembelea tovuti mara kwa mara ikiwa ni pamoja na madiwani kufanya kazi mara nyingi na Afisa habari huyo.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya kigoma ujiji aliwashukuru viongozi hao kuja kutembelea manispaa kwa lengo la kuleta ufanisi wa kazi hasa maeneo ya malalamiko, upande wa tovuti, mapato na maadili kwa watumishi na kuendelea kusema ushauri walioutoa utasimamiwa kwa uzuri na kufanyiwa kazi.
Viongozi hao wapo manispaa mkoani Kigoma kwa siku tano ambapo watapita katika kata mbalimbali wakiangalia utendaji kazi wa kamati za malalamiko na na namna ya kushugulikia malalamiko hayo
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa