Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amezuia kaguzi zilizokuwa zikifanywa na Maafisa Mapato na Biashara kwa Wafanyabiashara wa nyumba za kulala wageni kwa lengo ukusanyaji Mapato.
Zuio hilo amelitoa Leo July 04, 2024 katika Kikao alichokifanya na Viongozi wa Wamiliki wa nyumba za kulala wageni, Wamiliki wa nyumba za kulala Wageni pamoja na Uongozi wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Mkoani Kigoma (TCCIA).
Katika Kikao hicho Mkurugenzi wa Manispaa amesema ili kuendelea kuboresha Mazingira rafiki ya kibiashara kwa nyumba za kulala wageni, Wafanyabiashara hao watakuwa wakiwasilisha vitabu lengo la uhakiki na ulipaji kodi.
Amesema kusitishwa kwa kaguzi hizo kutapunguza vitendo vya rushwa na kuepuka usumbufu kwa wateja wanaolala katika nyumba hizo ikiwa ni pamoja na kukuza mahusiano baina ya Taasisi na Wafanyabiasha.
Amewataka kuwa waaminifu na kufuata taratibu, kanuni na sheria ikiwemo kuandika majina ya wateja, kuzingatia Usafi na usalama wa Wateja wao.
Aidha amewataka wale waliojenga Majengo kwenye maeneo ya makazi kuwasilisha maombi ya mabadiliko ya matumizi ya ardhi ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma za lesseni na huduma zingine kupitia mifumo ya kielektroniki.
Kikao hicho ni cha kwanza kwa kundi la Wafanyabiashara ambapo ameahidi kuendelea kukutana na Makundi Mengine ya Wafanyabiashara na Wajasiriamaili waliopo katika Manispaa hiyo.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa