Kaimu mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Jabir Majid leo January 17, amezitaka asasi zisizo za serikali kutoa taarifa za fedha kwa uwazi kwa serikali na wananchi wanaowahudumia kutokana na fedha wanazozipokea kutoka kwa wafadhili wao.
Ameyasema hayo katika kikao cha halmashauri kikiwa na wadau wa asasi hizo zisizo za kiserikali (NGO’s) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano mkoani, na kikiwa kimefunguliwa na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Bennert Ninalwo.
Kaimu mkuu wa idara ya maendeleo jamii huyo amesema “Asasi hizi za zisizo za serikali lazima mhakikishe mnatoa taarifa kwa ngazi husika kupitia Ofsi ya Mkurugenzi na haya ni Maagizo kutoka mamlaka za juu kwamba taarifa zote zianzie ngazi ya Halmashauri tena kwa Uwazi”.
Akizungumzia suala la taarifa ya fedha ambazo asasi zisizo za kiserikali wanazozipata amesema taarifa inatolewa kwa wale wanawahudumia pamoja na ofsi ya Mkurugenzi kupitia ofsi ya Maendeleo ya Jamii na pale asasi inapopata zaidi ya shilingi million 20 ni lazma fedha hizo zitangazwe katika vyombo vya habari ambapo wananchi au wanufaika watapata taarifa kwa urahisi.
Ameendelea kuzitaka asasi hizo zisizo za Serikali kuendelea kufanya kazi zilizopo katika maandiko yao na kufanya kazi ya kuongeza kipato cha asasi hizo ili ziweze kujiendesha bila kutegemea wafadhili na kutogawana faida inayopatikana bali kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi.
Ameendelea kusema asasi zisizo za kiserikali lazma iwe na eneo la Ofsi linalotambulika, kuhakisha wanalipa ada za kila mwaka, kuwa na mpango kazi na bajeti pamoja na kutumia wataalamu mbalimbali katika shughuli ambazo zinafanywa na asasi hizo..
Naye afisa maendeleo ya Jamii wa manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Radan Lameck amewakumbusha wadau na wasimamizi wa asasi hizo zisizo za kiserikali kutekeleza masuala mtambuka na kuzipa kipaumbele katika shughuli wanazozifanya
Masuala hayo mtambuka ni pamoja na kuzungumzia suala la UKIMWI huku wakikumbusha wananchi kwamba ugonjwa huo upon a kuwekea bajeti juu ya yelimishaji wa ugonjwa huo,
Ameendelea kusisitiza asasi hizo kuwawezesha wananchi katika masuala ya Kiuchumi katika sekta mbalimbali kama vile kilimo na biashara huku wakikumbusha sera ya nchi kwa kipindi hiki ikiwa ni serikali ya viwanda na kufikia uchumi wa kati na vijana kukumbushwa suala la kuwa wabunifu katika ukuzaji wa teknolojia na elimu ya kujiajiri.
Amemalizakwa kuhimiza asasi hizo kutoa elimu ya lishe kwa wananchi wanaowahudumia ikiwa ni vyenzo ya kuondoa na kupunguza udumavu kwa halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa wakazi kuhakikisha wanapata chakula bora chenye virutubisho .
Nao wadau kutoka katika asasi ziziso za kirai (NGO’s) wakichangia katika mkutano huo mmoja wa washiriki kutoka asasi ya NDELA amewapongeza kwa taarifa na mambo yaliyoelezwa huku wakiahidi kuyafanyaia kazi katika asasi aliyopo na kuwataka wataalamu kutoka ofsi ya Mkurugenzi kutembelea asasi hizo katika maeneo yao wanayofanyia kazi na kutokaa ofsini tu.
Naye Bi. Shida Selemani aliyejitambulisha kama mama anayeishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU)na kufanya kazi ya kuelimisha namna ya kujikinga na virusi hivyo na kwa wale wanaosambaza virusi amezitaka asasi mbalimbali na serikali kuwapatia ofsi ikiwa ni changamoto inayowakabili kwa kukosa ofsi ya kudumu ikiwa kwa sasa wamesaidiwa na asasi ya NDELA kwa kuwapatia ofsi kwa mda.
Mkutano huo uliochukua takribani masaa manne uliohudhuliwa na asasi zizizo za serikali zaidi ya ishirini ulimalizika kwa kufungwa na Mratibu wa Vijana wa mkoa wa Kigoma Ndugu . Edward Manase kwa kusema maoni yana yohusu upande wa serikali yamechukuliwa na yatafanyiwa kazi.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa