Na Mwandishi wetu
Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma leo Februali 5, 2021 imefanya ziara Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa lengo la kukagua Utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa mwaka 2015-2020
Ziara hiyo imefanyika ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Kigoma Ndugu. Amandus Nzamba akiongozwa na kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kigoma na Wataalamu wa Manispaa ya Kigoma /Ujiji
katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma amekabidhi Madawati na Meza mia moja hamsini (150) kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Kigoma Ujiji baada ya kufika kutembelea ukarabati na Ujenzi wa Shule hiyo uliogharimu Kiasi cha Fedha Million Sitini na nane na eĺfu sabini (608,070,000/=) ikiwa ni mapato ya Ndani ya Halmashauri hiyo
Aidha Mwenyekiti huyo amefika kuwasikiliza wananchi wa Kata ya Bangwe wenye Mgogoro wa ardhi ambapo wamedumu na Mgogoro huo kwa mda mrefu bila kupatiwa majibu huku Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Manispaa hiyo Ndugu. Brown Nziku akisema Mgogoro huo tayari upo kwa Kamishina wa ardhi Kanda ya Magharibi na mwekezaji wa eneo hilo amesitishwa kwa ujenzi aliokuwa akiufanya hadi pale jambo hilo litakapotatuliwa na kupatiwa ufumbuzi
Katika ziara iliyofanyika na kamati ya Siasa ya Mkoa wa Kigoma ya Chama Cha Mapinduzi maeneo mengine waliyo tembelea ni pamoja na Chanzo cha maji Bangwe, Ujenzi wa Jengo la Kujifungulia na Upasuaji Kituo cha Afya cha Gungu, na Dampo la Kisasa la Msimba mwenyekiti huyo amewataka Wataalamu kufanya kazi kwa weredi na kufikia Malengo yaliyokusudia na Kupata Maendeleo kwa Wakazi wa Manispaa hiyo
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu. Frednand Filimbi amempongeza Kiongozi huyo na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma na kamati yake kwa kutembelea Miradi huku akiahidi kufanyia kazi ushauri uliotolewa na kuendelea kusimamia Shughuli za serikali na Kuleta Maendeleo kwa Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa