Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amesema Vijana wenye umri wa miaka arobaini na tano (45) kushuka chini wanaruhusiwa kuunda Kikundi na kukopa katika mikopo ya 10% inayotolewa na Halmashauri kwa Makundi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Ameyasema hayo Leo Desemba 04, 2025 alipokuwa katika kipindi cha #Sikumpya kinachorushwa na Main FM iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Amesema Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeendelea kutoa mikopo ambapo katika kipindi hiki fedha za awali zilizotolewa ni Millioni hamsini na Sita (Tsh 56,000,000/=) na zaidi ya Millioni Mia tano (Tsh 555,652,400/=) zimetolewa hivi karibuni.
Amesema tayari Halmashauri imetangaza Utoaji wa mikopo isiyokuwa na riba kiasi cha Million Mia nne arobaini ( Tsh 440,000,000) huku akitaka makundi hayo kuanza kuomba.
Amesema kwa sasa Manispaa hiyo inashirikiaba na Bank ya CRDB kutoa elimu ya kifedha katika Makundi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa