Na Mwandishi wetu
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigoma Leo Desemba 30, 2021 imefanya ziara ya kutembelea ujenzi wa Madarasa arobaini na nane (48) uliokuwa unaendelea kwa Shule za Sekondari kumi na Sita (16) Manispaa ya Kigoma/Ujiji huku ikiridhishwa na Ubora na viwango vya ujenzi huo
Ziara hiyo imefanyika ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Kigoma Ndugu. Alhaji Yassin Mtalikwa ambapo amesema Lengo la ziara hiyo ni kukagua, kusimamia na kujiridhisha na Utekelezaji wa Ilani kwa viwango na ubora unaohitajika
Aidha Mwenyekiti huyo amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigoma imefanya ukaguzi wa miradi hiyo na kujiridhisha na usimamizi uliofanyika na Wataalamu huku akisema madarasa hayo yapo katika viwango vilivyowekwa kutokana na makisio yaliyotolewa na Wahandisi wa Ujenzi
Mwenyekiti huyo wa Wilaya amempongeza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za Ujenzi huo akishirikiana na Shirika la Fedha IMF Kwa kutoa fedha hizo huku akisema miundombinu hiyo itaboresha Mazingira ya Ufundishaji na Ujifunzaji
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athuman Msabila amesema mafanikio ya Ujenzi huo kwa wakati imechagizwa na kamati za usimamizi zilizoundwa na ununuzi wa vifaa vya ujenzi uliofanyika mapema huku akisema wanafunzi wote wa Kidato cha kwanza wataochaguliwa wataanza masomo kwa wakati mapema mwezi Januari 2022
Manispaa ya Kigoma/Ujiji ilipokea kiasi cha fedha za Kitanzania Million Mia tisa sitini (960,000,000/=) kutoka Serikali Kuu kutokana na Mkopo uliotolea wa Shirika la Fedha IMF ili kujenga vyumba vya madarasa arobaini na nane (48) kwa shule za Sekondari kumi na sita (16) ikiwa ni jitihada za kuinua Uchumi na kupambana athari za Uviko-19 Nchini Tanzania
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa