Na Mwandishi Wetu
Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigoma leo June 13, imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya chama hicho Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kipindi cha mwaka mmoja July 2020 hadi June 2021 na kuridhishwa na miradi iliyotekelezwa
Ziara hiyo imefanyika ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho wilaya Alhaji Yassin Mtalikwa ambapo wajumbe wa kamati hiyo wamepongeza ubora wa viwango wa miradi inayoendelea kujengwa chini ya usimamizi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Katika ziara hiyo jumla ya miradi yenye zaidi ya thamani ya Fedha za Kitanzania Million mia saba (700,000,000/=) imekaguliwa huku Mwenyekiti huyo akipongeza usimamizi unaofanyika na Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo
Mwenyekiti huyo akiwa katika Zahanati ya Rusimbi ambapo Ujenzi wa wodi ya wazazi unaendelea amewapongeza Wananchi wa Kata hiyo kwa kuunga juhudi ya ujenzi kwa kuchangia kiasi cha fedha za Kitanzania Million saba laki saba elfu sitini na moja na mia tano ( Tsh 7,761,500/=) huku Serikali ikitoa Kiasi cha million hamsini (Tsh 50,000,000/=) na kiasi cha Million kumi (Tsh 10,000,000/=) zikihitajika katika ukamilishaji wa Jengo hilo
Ameendelea kupongeza Wananchi wa Kata ya Katubuka kwa ujenzi wa msingi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Majengo na Serikali ikitoa kiasi cha fedha Million hamsini (Tsh 50,000,000/=) katika ukamilishaji wa vyumba hivyo huku akiwataka wakazi wote wa Manispaa hiyo kuendelea kuchangia nguvu kazi na fedha katika miradi inayotekelezwa katika maeneo yao
Miradi mingine iliyotekelezwa ikihusisha nguvu ya wananchi ni pamoja na ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasa na ofisi za walimu mbili (2) Shule ya Msingi Kabingo na Serikali ikitoa fedha za Kitanzania Million hamsini (Tsh 50,000,000/=) katika ukamilishaji wa ujenzi huo, Ujenzi wa Zahanati ya Buronge na Serikali ikitoa fedha za Kitanzania Million thelathini (Tsh 30,000,000/=) katika ukamilishaji wa Ujenzi huo
Akihitimisha ziara hiyo Mwenyekiti huyo amewataka Wataalamu kuendelea kusimamia miradi katika viwango vinavyotakiwa ili iweze kunufaisha wakazi wa wote wa Manispaa hiyo na kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi kwa kupokea maoni na ushauri katika miradi mbalimbali
Naye kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Frednand Filimbi ameishukuru kamati ya Chama Cha Mapinduzi kwa kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali huku akisema Ofisi ya Mkurugenzi ikishirikiana na wataalamu itaendelea kusimamia miradi katika viwango bora na kuendelea kutatua kero za wananchi
Aidha Miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na ukamilishaji wa maabara mbili (2) za masomo ya Sayansi shule ya sekondari Kichakachui wenye thamani ya fedha za Kitanzania Million sitini (Tsh 60,000,000/=), Ujenzi wa Bweni moja wenye thamani ya fedha za Kitanzania Million themanini (80,000,000/=) ujenzi wa madarasa mawili yenye thamani ya fedha za Kitanzania Million arobaini (Tsh 40,000,000/=) maabara mbili (2) yenye thamani ya fedha za Kitanzania Million sitini (Tsh 60,000,000/=) katika shule ya Sekondari Kasingirima, Ujenzi wa Bweni Shule ya Sekondari Buronge yenye thamani ya fedha za Kitanzania Million themanini (Tsh 80,000,000/=) ,Ujenzi wa Machinjio ya Ujiji Kisasa wenye thamani ya Fedha za Kitanzania Million mia moja na themanini na mbili (Tsh 182,913,668/=) na kutembelea kitalu cha miche ya Michikichi ya kisasa kilichopo eneo la Katosho
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa