Na Mwandishi Wetu
Kamati ya usalama ya Wilaya ya Kigoma ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Dr. Rashid Chuachua Leo Januari 27, 2025 imepata mafunzo ya elimu ya uraia na utawala bora.
Mafunzo hayo yametolewa na Wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria yakihusisha washiriki wengine Wakuu wa Idara na Vitengo na Watendaji Kata Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Wakufunzi wa Mafunzo hayo wamesisitiza Viongozi kuzingatia nguzo za utawala bora katika kuwahudumia wananchi ikiwemo Uwazi, uwajibikaji, Utawala wa Sheria, Usawa na Uadilifu.
Mada mbalimbali zimewasilishwa ikiwemo Wajibu wa Viongozi katika kudumisha demokrasia, Kusimamia na kudumisha amani na utulivu wa Nchi, kuimarisha Ulinzi na usalama kwa ushirikiano baina Viongozi na Jamii, kuboresha utoaji wa huduma kwa Wananchi na kuzingatia haki za binadamu.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa