Kamati ya wilaya ya mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili wa wanawake na watoto (MTAKUWWA) kwa mara ya kwanza jana Desemba 5, ilikutana katika ukumbi mdogo wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji kujadili na kuweka mikakati na maazimio ya kuhakikisha vitendo hivyo vinatoweka.
Akifungua kikao hicho kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji Ndugu. Berneth Ninalwo aliwataka wajumbe wote waliohudhulia kikao hicho kuhakikisha inawekwa mipango thabiti kukahakikisha vitendo hivyo vinatoweka na kuwa agenda ya kudumu katika kupinga vitendo vya ukatili kuanzia ngazi ya familia.
Katika kikao hicho wajumbe waliweza kusomewa majukumu ya kamati hiyo na katibu wa MTAKUWWA wilaya Bi. Agnes Sanga ikiwa ni pamoja na kamati kutekeleza mpango kazi wa kitaifa wa kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, na kuhamasisha na kutoa elimu juu ya kutokomeza ukatili wa wanawake na watoto.
katika kikao hicho mwenyekiti aliweza kukaribisha wajumbe na wadau mbali mbali kutoa taarifa namna wanavyofanya kazi katika kuhakikisha vitendo vya ukatili wa wanawake na watoto vinatoweka katika wilaya na halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Akitoa taarifa Afisa wa Polisi dawati la kupinga ukatili wa wanawake na watoto Bi. Mary Paul aliweza kueleza majukumu yanayotekelezwa na jeshi la Polisi ikiwa ni kupokea taarifa za ukatili mbali mbali ikiwa ni pamoja na ubakaji, kupigwa , kuchomwa moto kwa watu wanaofanya vitendo hivyo vya ukatili.
Aliendelea kutoa taarifa kuwa kwa mwaka huu mpaka sasa wamepokea kesi 20 za kubaka, kesi 1 ya kupapaswa kwa mtoto wa kike na dereva bajaji, kesi 15 za migogoro ya kifamilia ikiwemo kutelekezwa kwa wanawake na watoto na tayari zimeshafikishwa Mahakamani na dereva bajaji amehukumiwa miaka 5 jera, na hadi hivi sasa wanaendelea kutoa eli mu juu ya kupinga na kutokomeza vitendo vya Ukatili wa wanawake na watoto mashuleni ikiwa ni pamoja na shule ya msingi ya Bangwe, shule ya msingi ya Muungano, shule ya upili ya Kitwe, shule ya upili ya Mlole na shule ya upili ya St. James huku akieleza changamoto ni watu wengi kutoripoti vitendo hivyo vya ukatili na kuamuliwa ngazi ya familia.
Naye kiongozi kutoka taasisi ya Living Soul Foundation inayojishughulisha na u na ulinzi wa watoto na kupinga ndoa za utotoni Bi. Happines Nkorogo akitoa taarifa za taasisi yake alisema wameweza kufanya uelimishaji wa wanafunzi mashuleni vya kuhakikisha vitendo hivyo vya ukatili kwa wanawake na watoto vinatoweka kabisa baahi ya shule ni pamoja na shule ya upili ya Kichakachui, shule ya upili ya Katubuka, kitongoni na shule ya upili ya Kitwe.
Aliendelea kusema lengo kubwa ni kuhakikisha mtoto na mtoto wa kike wanakuwa salama na kufikia ndoto zake licha ya changamoto ambayo watoto wa kike ni kupewa kazi nyingi za nyumbani tofauti na watoto wa kiume na wazazi wanapongombana watoto hutelekezwa na kubaki na malezi yasiyo ya wazazi wote.
Wadau wengine waliotoa taarifa ni pamoja na Kenneth Hageze kutoka taasisi ya Sanganigwa ya kulea watoto yatima, Betrida Buhaga mratibu wa taasisi ya MAPAO inayojishughulisha na usaidizi wa kisheria , elimu na utatuaji wa migogoro, kiongozi kutoka ofsi za Uhamiaji ndugu. Ally Hadivumi wakiwemo wataalamu kutoka ofsi ya mkurugenzi.
Baada ya kuwasilisha taarifa za utendaji kazi kutoka kwa wadau mbalimbali kamati iliweza kujadili na kuweka maazimio ya utekelezaji katika shuguli za utekelezaji ikiwa ni pamoja na taarifa za wadau na wataalamu kuhakikisha zinawasilishwa zikiwa na takwimu halisi kutoka katika maeneo wanayofanyiwa kazi,na kuhakikisha wadau hao wanapofanya kazi kushirikisha vyombo vya habari ili kuhakikisha elimu inawafikia wananchi kwa urahisi zaidi.
Kikao hicho kilichoanza majira ya saa nne asubuhi kiliweza kufungwa na mwenyekiti wa kikao hicho kwa kuwashukuru wote waliohudhuria na kuwataka wadau wote kushirikishana katika shughuli wanazokuwa wanazifanya kila siku na kuendelea kuhamasisha wananchi kuhakikisha wanaripoti na kutoa taarifa vitendo vya ukatili katika mamlaka husika pindi vitendo hivyo vinapotokea.
Picha zaidi za habari hii nenda katika maktaba ya picha.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa