Na Mwandishi wetu
Kamati zinazoshughulika na kutokomeza Ukatili wa dhidi ya Wanawake na Watoto(MTAKUWWA) Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma zatakiwa kuibua mbinu za uibuaji matukio ya Ukatili yanayofanyika Ndani ya Halmashauri hizo
Kamati hizo za Halmashauri zilitakiwa hivo Jana Septemba 14, katika Ukumbi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji zilipotembelewa na Kamati ya kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ngazi ya Mkoa ikiongozwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Ndugu. Moses Msuluzya ikiwa na lengo la kukagua namna kamati za Halmashauri zinavyofanya kazi
Akiongea na Kamati hizo Kaimu Katibu Tawala huyo alisema kwa sasa Katika Mkoa wa Kigoma unachangamoto ya Vitendo vya ukatili vinavyofanya kutolipotiwa na badala yake kusuluhishwa ndani ya Jamii na familia hali inayofanya kuathirika kwa wahanga na jamii kukithiri na kuongezeka kwa vitendo hivyo
Katibu Tawala huyo aliitaka Kamati hiyo kuibua mbinu mpya kwa kuendelea kutoa elimu ndani ya jamii katika maeneo ambayo vitendo hivyo vya ukatili vimekithiri na kutoa mawasiliano kwa maafisa Ustawi wa Jamii na Dawati la Jeshi la Polisi ili vitendo hivyo kuweza kuripotiwa
Aliendelea kusema elimu na kujitambua kwa jamii ndicho kitu kitakacholeta mabadiliko makubwa ndani ya Jamii huku akizitaka kushirikiana na idara zingine kama idara ya Elimu Msingi na Sekondari katika kuhakikisha vitendo vya ukatili vinapungua na kuisha katika Halmashauri zote mbili
Awali akisoma taarifa ya namna Kamati ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji inayoshughulikia Kutokomeza, vitendo vya Ukatili wa Wanawake na Watoto Afisa Ustawi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Agnes Punjila alisema Jamii na wakazi wa Manispaa hiyo wamekuwa wakipata elimu ya namna kupinga Ukatili wa Wanawake na Watoto huku jamii hiyo ikatakiwa kutoa taarifa ya kuripoti kwa wakati vitengo hivyo vya ukatili
Akitoa takwimu za vitendo walivyoshughulikia katika Manispaa hiyo kwa kipindi cha Januari hadi June 2020 alisemà vitendo vilivyolipotiwa vya ukatili ni Watoto mia moja arobaini na moja (141) wakitelekezwa na wazazi wao, huku Watoto wanaofanya kazi mtaani wakiwa ni watoto wa kike 44 , mtoto wa kiume akiwa mmoja ukatili wa Kimwili ikiwa ni pamoja na Kipigo na kuchomwa na vitu vyenye Ncha kali wanawake nane (08), huku wanaume wawili (02) wakifanyiwa ukatili huo
Aliendelea kutoa takwimu za mashauri ya ukatili dhidi ya Wanawake yaliyoshughulikiwa ni pamoja na matunzo ya watoto mia moja arobaini na moja (141), Utatuzi wa migogoro ya Ndoa thelathini na tano (35), kuripotiwa kwa Mimba nane (08) za wanafunzi, kesi za watoto zilizopo Gereza la Bangwe zikiwa kesi tatu (03), huku kesi zilizopo katika mahakama ya Watoto zikiwa kesi nane (08)
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Zilipa Kisonzera Akitoa takwimu za Hali ya ukatili kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2020 na namna walivyoshughulikia alisema jumla ya Mashauri dhidi ya watoto yaliyofanyiwa kazi kwa miezi sita yalikuwa 121 huku mashauri dhidi ya wanawake 22 yakishughulikiwa na Watoto walioathirika na vitendo výa ukatili yaliyoshughulikiwa wakiwa wavulana 47, Wasichana 74 na wanawake 22
Aidha wawasilishaji wote wa Halmashauri hizo walisema kwa sasa wanakumbana na changamoto ni Jamii kutotoa ushirikiano pindi kesi hizo za vitendo vya ukatili zinapopelekwa Mahakamani hasa kesi za ubakaji na ulawiti, changamoto nyingine ikiwa ni kukosa kituo cha pamoja (One stop Centre) kwa ajili ya kuharakisha kesi za ukatili
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu Mwailwa Pangani akizungumza katika kikao hicho aliishukuru kamati hiyo ya MTAKUWWA ngazi ya Mkoa kwa kutembelea kamati hizo za Halmashauri Mbili huku akiwaahidi kuendelea kuimarisha kwa kamati ya MTAKUWWA Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kuiwezesha kupambana na vitendo vya ukatili kwa kupatiwa mafunzo na kuendelea kuelimisha jamii kuachana na vitendo hivyo vya ukatili kutokana na athari zake
Picha na video zaidi ingia Maktaba ya picha www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa