Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro Leo Januari 24, 2025 amezindua kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MAMA SAMIA Legal Aid Campaign)
katika Uwanja wa Mwanga Community centre Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Akihutubia katika uzinduzi huo amesema kampeni inalenga katika kutoa elimu na utatuzi wa migogoro katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo Migogoro ya ardhi, Ukatili wa kijinsia, mirathi, ndoa na masuala ya uraia.
Amesema huduma hiyo inatarajia kufanyika kwa mda wa Siku tisa (09) kwa Halmashauri Zote za Mkoa wa Kigoma ambapo Wataalamu wakiwemo Mawakili watapita katika Mitaa, Vitongoji na vijiji katika kutatua Changamoto zinazowakabili Wananchi.
Amesema huduma hizo zinatolewa bure ikiwa ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassani kila Mwananchi anapata Haki na kwa wakati kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa