Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kushirikiana na Wadau wa Mazingira, Wananchi na Watumiaji wa mialo na fukwe za Ziwa Tanganyika inatarajia kuanza kampeni ya Usafi na usafi wa mialo na fukwe kwa mda wa siku saba (07) ili kuepuka athari za uchafuzi wa maji na viumbe hai
Kampeni hiyo inatarajia kuanza mapema Kesho March 15, 2023 Katika Mwalo wa Katonga ambapo wadau wa Mazingira, Wavuvi, Wafanyabiashara wa Mazao ya Uvuvi, Vyama vya uratibu wa mwalo na Wananchi wanatarajia kujitokeza kufanya Usafi kwa kuokota taka ngumu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji inatarajia kushirikiana na Wahadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma na taasisi ya inayohusika na Mazingira na ukuzaji uchumi(EMEDO) kwa kutoa elimu ya umuhimu wa kuwa na fukwe na mialo salama ambapo pia wanatarajia kutoa elimu ya uchumi rejereshi
Mratibu wa kampeni hiyo kutoka Environmental management and economic development organizations (EMEDO) Ndugu. Arthur Mugema amesema kampeni hiyo ya Usafi na Usafi itafanyika katika fukwe kumi na tano (15) za ziwa Tanganyika na kutoa elimu kuwa na usafi endelevu
Katika zoezi hilo Wananchi watapata elimu na kuongeza uelewa wa utunzaji mazingira na kujengewa tabia endelevu ya Usafishaji ili kuongeza mazalia ya Samaki, na kukuza uchumi wa Wananchi
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa