Na mwandishi wetu
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Frednand Filimbi akiambatana na baadhi ya Wakuu wa idara na Vitengo leo May 20, 2021 amefanya ziara katika Kata ya Kipampa ambapo shule ya sekondari inatarajiwa kujengwa na Wafadhili wazawa
Akiwa katika eneo hilo linalotarajiwa kujengwa Kaimu Mkurugenzi huyo amekutana na Diwani wa Kata hiyo ambaye ni Naibu Meya Mhe. Mgeni Kakolwa (Bi) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Mji, Ujenzi na Mazingira Mhe. Himidi Omary Himidi pamoja na watendaji wa kata hiyo
Kaimu Mkurugenzi huyo amemtaka Mtendaji wa kata hiyo kufanya usafi wa eneo hilo na kutoa elimu kwa wakazi wa kata hiyo kushiriki katika ya shughuli hiyo ya maendeleo huku akiwataka kusimamia ujenzi huo utakao anza hivi karibuni
Wafadhili hao ambao ni wazaliwa wa Ujiji wanatarajia kujenga vyumba vinne (04) vya madarasa pamoja na vyoo na Shule hiyo inatarajiwa kujengwa nyuma na jirani ya shule ya msingi Ujiji ilipo na tayari nguvu ya wananchi ilikuwa ilishaanza kutumika kwa kujenga misingi ya baadhi ya vyumba vya madarasa
Aidha Mkurugenzi huyo ametembelea na kukagua ujenzi wa bwalo ulioanza katika shule ya sekondari Kasingirima ikiwa ujenzi huo unafadhiliwa na wafadhili hao , Mkurugenzi amemtaka Mhandisi wa Manispaa hiyo kusimamia ujenzi huo huku akiwapongeza wafadhili hao na kuwataka wazaliwa wa Manispaa hiyo wanaoishi Ndani na Nje ya Nchi kuwa kielelezo kwa kuweka alama kwa kujenga miundombinu ya huduma za jamii
Manispaa ya Kigoma/Ujiji ina jumla ya kata kumi na tisa (19), kwa sasa kata nne (04) zinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa shule za sekondari za kata ambazo kata hizo ni pamoja na kata ya Kipampa, Businde, Katubuka, na kata ya Kigoma
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa