Na Mwandishi wetu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Rashidi Mchatta leo June 9, 2021 amefungua Mashindano ya michezo kwa Shule za Sekondari (Ummiseta) yaliyoanza kwa ngazi ya mkoa katika Uwanja wa chuo cha walimu kasulu
Akifungua Mashindano hayo Katibu Tawala huyo amewaagiza wataalamu wa Mkoa huo kuja na andiko la kuanzisha shule au kituo cha michezo (Centre of Sports Academy) na baada ya miezi mitatu wataalamu hao wawe wamewasilisha majibu ofisini kwake juu ya utekelezaji wa agizo Kwa lengo la kukuza vipaji vilivyopo Mkoani hapo
Amewapongeza Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Elimu, Maafisa Michezo ,Walimu wa Michezo na Wanamichezo wote tangu walipoanza Mashindano kwa ngazi ya Shule, Kata hadi ngazi ya Wilaya na sasa kushiriki katika Mashindano ngazi ya Mkoa
Aidha amewataka Walimu na wakufunzi wa michezo kuchagua wana michezo bora katika kuunda timu ya Mkoa watakaoleta ushindi kwa Mkoa wa Kigoma kwa michezo yote na kutozingatia usawa wa kuchagua wachezaji kutoka katika kila Halmashauri
Akihutubia katika uwanja huo amesema wanamichezo wana nafasi kubwa katika kufanya vizuri katika masomo ya darasani huku akiwataka wanafunzi hao wa Shule za Sekondari kuzingatia pia masomo huku wakikuza vipaji walivyonavyo
Afisa elimu Mkoa wa Kigoma Ndugu. Omary Mkombole Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi alisema wapo wanamichezo mia saba (700) wanaoshiriki kutoka katika Halmashauri nane (8) za zinazounda Mkoa huo ,huku akisema wanaimani watapata wachezaji bora watakaoishiriki ngazi ya Taifa na kuiletea ushindi Mkoa wa Kigoma
Mashindano hayo ya ngazi ya Mkoa yenye lengo la kupata timu bora zitakayoshiriki kwa ngazi ya Taifa katika Michezo mbalimbali yatafanyika kwa siku nne (4) ambapo yanatarajia kukamilika June 11, 2021 na Michezo itakayofanyika ni pamoja na Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Mikono, Mpira wa Wavu, Mpira wa Kikapu, Riadha na Mashindano ya fani za ndani yaani Kwaya na Ngoma na Kitaifa Mashindano haya yanatarajiwa kufanyika Mkoani Mtwara
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa