Na mwandishi wetu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Rashidi Mchatta siku ya Ijumaa Novemba 20, alifanya ziara kwa kutembelea vikundi viwili (2) vya wajasiliamali walemavu Manispaa ya Kigoma/Ujiji kukagua shughuli wanazozifanya katika uzalishaji Mali
Kiongozi huyo alifanya ziara hiyo ikiwa ni mwendelezo wa ziara aliyoifanya katika Halmashauri zote za Mkoa wa Kigoma akikagua utekelezaji wa shughuli za shirika la Help Age namna inavyosaidia na kuinua uchumi wa watu wenye ulemavu katika Mkoa huo
Kiongozi huyo alitembelea kikundi cha Nyota Njema kinachojishughulisha na utengenezaji wa sabuni katika eneo la Sido na kutembelea kikundi cha Umoja wa watu wenye Ulemavu Burega wanaojishughulisha na uzalishaji wa chakula cha kuku kwa kutumia magamba ya konono
Akiwa katika ziara hiyo Katibu Tawala huyo aliipongeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kuviwezesha vikundi hivyo vya Wajasiliamali walemavu kwa kila kikundi kukopeshwa mkopo wa Masharti nafuu na kila kikundi kupata kiasi cha Millioni Tano (5,000,000/=) kutokana na asilimia kumi ya mapato ya Halmashauri ya kuviwezesha vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu
Aidha kiongozi huyo aliipongeza shirika la Help Age kwa namna inavyosaidia kuinua vikundi hivyo huku akiwataka wataalamu wa Maendeleo ya Jamii kuvitembelea vikundi hivyo mara kwa mara ili kujua maendeleo yao na kutoa semina za shughuli wanazozifanya ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zilizopo katika vikundi hivyo
Mhasibu wa kikundi cha Nyota Njema na Mlemavu wa Miguu Bi. Akizimana Emmanuel alishukuru Òfisi ya Mkurugenzi kwa Mchango wa kupatiwa Mkopo wa masharti nafuu huku akisema wamekuwa wakinufaika katika Shughuli hizo wanazozifanya kwa kuhudumia familia zao kutokana na kipato wakipatacho
Naye Mwenyekiti Msaidizi wa Kikundi Cha Umoja watu wenye Ulemavu Burega Ndugu Buhungu alimpongeza kiongozi huyo kwa kuwatembelea huku akiwataka wale wote wenye ulemavu kufanya kazi Mbalimbali za kiuchumi na kuachana na dhana ya Mlemavu kuwa omba omba
Kwakipindi cha robo ya kwanza na ya pili(Julai-Novemba, 2020) Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeviwezesha vikundi vya wajasiliamali Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu mikopo isiyo kuwa na riba Kiasi cha Fedha Million thelathini na nne ( Tsh 34, 000,000/=) kutokana na asilimia kumi inayotengwa kwa ajili ya kuwezesha makundi hayo
Picha zaidi ingia maktaba ya picha
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa