Katibu tawala wa mkoa wa Kigoma Ndugu. Rashid K. Mchata amewataka wakazi wa mkoa wa Kigoma kutumia fursa ya siku tatu zilizoongezwa kwenda kujiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura ili kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa November 24
Aliyasema hayo jana October 13 katika ziara yake aliyoifanya ya kutembelea halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji na halmashauri ya Kigoma vijijini(kigoma dc) kukagua namna zoezi linavyofanyika katika vituo vya kujiandikishia
Akiwa katika halmashauri ya Kigoma vijijini msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa Bi. Petronila B. Gwakila alitoa taarifa na kusema uandikisha unaendelea vizuri ambapo hakuna changamoto yeyote iliyokwisha jitokeza katika uandikisha na maafisa uandikishaji walipata semina namna watakavyofanya kazi kwa kushirikiana na mawakala wa vyama vya siasa
Naye msimamizi wa uchaguzi manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Emmanuel Katemi akitoa taarifa wakiwa katika halmashauri hiyo alisema uandikishaji unaendelea vizuri na watu wamejitokeza kwa kiasi kikubwa ambapo alisema katika kituo cha kata ya ofisi ya kitongoni uandikishaji uko kwa asilimia 92 kwa makisio ya wapiga kura na kituo cha shule ya msingi Bangwe kikiwa na asilimia ya 60 ya makisio ya wapiga kura.
Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura Ndugu. Hamza Yassini na Bertha Musa wameweza kumpongeza katibu tawala huyo kwa ufuatiliaji anaoufanya na kusema wao tayari wamejiandikisha na wapo tayari kusubilia ratiba nyingine inayofuata na kueleza watashiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuchaguz na kugombea nafasi za uongozi.
Naye Katibu Tawala huyo amewapongeza wananchi kwa kujitokeza katika uandikishaji huo na kuwataka wananchi kuweza kujitokeza zaidi katika zoezi hilo kutokana na kuongezewa siku na waziri mwenye dhamana katika uandikishaji huo.
Aliwaasa waandishi na mawakala kutomkatilia mtu yeyote katika kujiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura kutokana na kuwa takwa la kikatiba kwa kila raia mwenye umri wa miaka 18 ila ni kufuata hatua za pingamizi kwa mtu anayetiliwa mashaka pindi uandikishaji huo utakapomalizika.
Alihihitimisha kwa kuipongeza wilaya ya Kakonko kwa kufikia asilimia sitini (60%) ya wapiga kura wote ambao wameshaandikwa katika daftari hilo la orodha ya upigaji kura na kuwataka wasimamizi hao wa uchaguzi kubuni mbinu bora za kuwafikia wananchi na uboreshaji wa matangazo ya sauti yanayokuwa yakipita mtaani katika kuwaelimisha wananchi
Uandikishaji huo wa orodha ya wapiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa ulianza October 8 ambapo ulitarajiwa kuhitimishwa oktoba 14 lakini kutokana na sababu zilizoelezwa na waziri wa TAMISEMI Mhe. Sulemani Jafo mikoa mingi nchini Tanzania mvua kunyesha kwa kiasi kikubwa na watu kushindwa kwenda kujiandikisha na sababu nyingine wananchi kuwa na dhana potofu ya mtu aliyejiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura kutojiandikisha tena katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa jambo ambalo sio sahihi.
Waziri hyo wa TAMISEMI ameongeza siku tatu (3) Kutokana na sababu hizo na kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2019 na matangazo ya Serikali Na 371,372,373 na 374 ya Mwaka 2019 Waziri mwenye dhamana na Serikali za mitaa ana mamlaka ya kutoa miongozo mbalimbali kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
picha zaidi ingia katika maktaba ya picha
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa